Upangaji uzazi

Ripoti:Wanawake na wasichana milioni 6 wanatumia njia za kupanga uzazi

Nchini Kenya mbinu za kupanga uzazi kutumia sindano ndizo zinazopendelea kwa asilimia 47.9

Muhtasari

 

  •  Serikali kwa sasa inatoa huduma za bure za upangaji uzazi katika vituo va afya vya umma .
  • Hata hivyo bado kuna ukosefu wa usawa katika kupata huduma za njia za  kupanga uzazi kwani asilimia 1806 ya wanawake wanataka kuzitumia lakini hawawezi kuzifikia huduma hizo .
Afya
Image: Yusuf Juma

  Takriban wanawake na wasichana milioni sita nchin Kenya wanatumia njia za kisasa za upangaji uzazi  ili kuzuia kupata uja uzito ripoti mpya imeonyesha .

 Idadi hiyo ni milioni 2 zaidi ya wanawake na wasichna milioni nne waliokuwa wakitumia njia za kupanga uzazi mwaka wa 2012 .

 Katika mwaka mmoja uliopita  wanawake hao wote na wasichana  walizuia mimba  milioni 2.2 zisizohitajika na kuepuka  kuavya mimba 503,000 kwa njia isio salama kulingana na ripoti hiyo .

 

 Ripoti hiyo iliyotolewa kwa ushirikianao wa mashirika ya   UNFPA, USAID, the Bill & Melinda Gates Foundation na afisi ya Uingereza kuhusu maendeleo  ya jumuiya ya madola  iligundua kwamba Kenya ni miongoini mwa mataifa ambayo wanawake wake wengi  wanatumia njia za kupanga uzazi barani Afrika

 Ripoti hiyo inaonyesha kwamba asilimia 57.8 ya wanawake walioolewa wapo chini ya mpango wa upangaji uzazi . Hata hivyo  ukijumuisha idadi ya wanawake wote wakiwemo wasio katika ndoa idadi hiyo inapungua hadi asilimia 42.5 . Kenya ilikuwa miongoni mwa nchi za kwanza kujitolea kuhusika na mpango wa FP 2020 ulipozinduliwa  mwaka wa 2012.

 Idadi ya sasa ya  asilimia 57.8 ni upungufu mdogo  kutoka asilimia 59 iliyosajiliwa mwaka wa 2018  ya idadi ya wanawake na wasichana wanaotumia njia za kisasa za upangaji uzazi .

 Serikali kwa sasa inatoa huduma za bure za upangaji uzazi katika vituo va afya vya umma .

Beth Schlachter,  mkurugenzi mkuu wa  ameisifu Kenya  kwa juhudi zake katika kuhakikisha kwamba huduma hizo zinapatikana kwa urahisi na bure . amesema hali iliboreshwa hata Zaidi wakati wa janga la Corona .

 Hata hivyo bado kuna ukosefu wa usawa katika kupata huduma za njia za  kupanga uzazi kwani asilimia 1806 ya wanawake wanataka kuzitumia lakini hawawezi kuzifikia huduma hizo .

Beth  ameongeza : “ kila siku unapopita kuna mamilioni ya wanaotaka kutumia njia za kupanga uzazi  ili kuamua hatima zao . Tunapoelkea mwaka wa 2030  tunafaa kuendelea na jitihada za kuboreka  na kujenga msingi kutumia vinavyofanya vyema ili kuhakikisha kwamba hakuna msichana anayeachwa nyuma’

 

 Nchini Kenya mbinu za kupanga uzazi kutumia sindano  ndizo zinazopendelea  kwa asilimia  47.9  ikifuatwa na  ile ya vibandiko  vikiwa na asilimia 18.2 ,tembe zikiwa nafasi ya tatu kwa asilimia 14.1, kuondolewa yao la uzazi  kwa asilimia 5.6  na mbinu  njia ya  Lactational Amenorrhea Method (njia ya kumnyonyesha mtoto)  kwa asilimia 0.3