Joto la corona Tanzania Marekani yazidisha tahadhari

Muhtasari

 • Hii inajiri wiki moja tu baada ya kuwashauri raia wake dhidi ya kusafiri kwenda nchi hiyo ya Afrika Mashariki.

 • Serikali ya Tanzania haijatoa idadi ya jumla ya kesi za Covid-19 au vifo tangu Aprili 2020.

Chanjo ya corona
Chanjo ya Covid 19 Chanjo ya corona

Serikali ya Amerika imebaini kuwa kuna visa vingi vya maambukizi ya Covid-19 nchini Tanzania.

Hii inajiri wiki moja tu baada ya kuwashauri raia wake dhidi ya kusafiri kwenda nchi hiyo ya Afrika Mashariki.

"Ubalozi wa Amerika unafahamu kuhusu ongezeko kubwa la idadi ya maambukizi ya Covid-19 tangu Januari 2021," Ubalozi ulisema.

Katika tahadhari ya kiafya, Marekani  ilisema kanuni na juhudi za kupunguza na kuzuia maambukizi ya Covid-19 nchini Tanzania hazijatiliwa maanani sana.

Serikali ya Tanzania haijatoa idadi ya jumla ya kesi za Covid-19 au vifo tangu Aprili 2020.

"Vituo vya huduma za afya nchini Tanzania vinaweza kuzidiwa haraka katika kushughulikia wagonjwa. Uwezo mdogo wa hospitali nchini Tanzania unaweza kusababisha ucheleweshaji huduma za matibabu ya dharura," ilisema Amerika.

Kiwango cha tahadhari ya kusafiri Tanzania ni Kiwango cha 3.

Kituo cha Udhibiti na Kuzuia Magonjwa cha Amerika kinasema kwamba wasafiri wanapaswa kuepuka safari zote kwenda Tanzania.

Ubalozi unaendelea kupendekeza kwamba watu wote wachukue tahadhari katika shughuli za kila siku.

Rais John Magufuli aliwahakikishia wakaazi milioni 58 kwamba hawahitaji kuwa na wasiwasi juu ya kufuata hatua za kuzuia Covid-19.