Mbunge Moses Kuria akamatwa na polisi

Muhtasari

• Mbunge huyo alithibitisha kukamatwa kwake kupitia ujumbe wake kwenye mtandao wa Facebook ingawa hakutaja sababu ya kukamatwa kwake.

Mbunge wa Gatundu Kusini Moses Kuria anazuiliwa katika kituo cha polisi cha Karuri baada ya kutiwa mbaroni siku ya Jumatatu jioni.

Inasemekana kwamba mbunge huyo alikamatwa pamoja na tariban watu wengine 30 kwa madai ya kwenda kinyume na kanuni za kudhibiti maambukizi ya Covid-19.

Mbunge huyo alithibitisha kukamatwa kwake kupitia ujumbe wake kwenye mtandao wa Facebook ingawa hakutaja sababu ya kukamatwa kwake.

Katika ujumbe wake alikuwa amesema kwamba angefikishwa mahakamani leo (Jumanne).

"Arrested! Held at Karuri Police Station. Kiambu Court tomorrow. Still- #MeneMeneTekel #FinishAndGo"

 

Seneta wa Murang'a Irungu Kang’ata na mwanablogi Denis Itumbi kupitia mtandao wa Twitter pia walithibitisha kukamatwa kwa Kuria lakini walidai kuwa kukamatwa kwake huenda kulichochewa kisiasa.