Mauaji baina ya wapenzi: Raila atamaushwa na ongezeko la visa

Muhtasari

• Raila alikemea visa hivyo akisema kwamba "maisha mengi yanapotea kila siku kulingana na ripoti za vyombo vya habari."

• Alisema 'vifo vya kutisha' vilikuwa vya kuhuzunisha, haswa baada ya mtu kuuteka moyo wa mwenzake kimapenzi na kisha anamgeuka na kumuua.

Crime scene
Crime scene

Kiongozi wa ODM Raila Odinga amelalamikia ongezeko la visa vya mauaji baina ya wapenzi.

Raila alikemea visa hivyo akisema kwamba "maisha mengi yanapotea kila siku kulingana na ripoti za vyombo vya habari."

Raila, akitaka kuwepo kwa mjadala wa dharura wa kitaifa kuhusu unyanyasaji wa kijinsia, alisema "...vitendo visivyo vya kawaidi vya mauaji haviwezi kugeuzwa kuwa vya kawaida."

“Janga hili lazima lifike mwisho. Ikiwa hamuwezi kupatanishwa, basi, ondoka na kuishi," kiongozi huyo wa ODM alisema katika taarifa siku ya Jumanne.

Alisema 'vifo vya kutisha' vilikuwa vya kuhuzunisha, haswa baada ya mtu kuuteka moyo wa mwenzake kimapenzi na kisha anamgeuka na kumuua.

"Ni bahati mbaya… badala ya kuendelea kuwathamini na kuwapenda, wengine ghafla hugeuka kwa fujo, na wakati mwingine huwaua kinyama," Raila alisema.

Visa vya wapenzi kugeukiana na kuumizana vimeongezeka sana, na vinaripotiwa karibu kila wiki.

Hivi majuzi huko Mbooni Mashariki, mwanamume mmoja alimkatakata mkewe hadi kufa juu ya mzozo wa ardhi.

Aliuawa na wanakijiji waliokuwa na hasira.

Mnamo Aprili 8, mwanamume mmoja alimuua mkewe mjamzito na watoto wawili kwa kutumia nyundo katika eneo la Mbeere Kusini.

Kilomita kadhaa kutoka eneo hilo siku hiyo, afisa wa GSU alimpiga mkewe risasi saba kabla ya kujigeuzia bunduki na kujiua baada ya ugomvi.

Hudson Wakise, kulingana na ripoti za polisi alikuwa na hasira kwa sababu Pauline Wakasa - mkewe wa miaka saba, alikuwa ameamua kutengana naye na kuhama nyumba yao ya ndoa.

Polisi mnamo Aprili 14 walipata mabaki ya mwanamke anayedaiwa kuuawa na mpenzi wake katika eneo la Witeithie huko Juja, kaunti ya Kiambu.

Gari la Evans Karani lilikwama kwenye matope na akakimbia, na kuuacha mwili ndani ya gari. Baba ya Nyokabi aliwaambia waandishi wa habari baada ya uchunguzi wa mwili kwamba mwili ulikuwa umeharibika vibaya ishara ya kuteswa kabla ya kuuawa.

Mfanyabiashara huyo wa Kiambu mwenye umri wa miaka 38 atafanyiwa uchunguzi wa kiakili baada ya kukiri kumuua msichana huyo.