Covid-19: idadi kubwa ya vifo yasababisha uhaba wa kuni kuchoma maiti Kariokor

Muhtasari

• Watu wa umri wa juu kutoka jamii ya Asia nchini wamekuwa miongoni mwa walioathirika zaidi na janga la Covid-19. Jamii hiyo kwa kawaida huteketeza miili ya wapendwa wao kuambatana na tamaduni zao.

JIVU KWA JIVU: Uchomaji wa mwili wa aliyekuwa wakili wa serikali Satish Gautama katika makaburi ya Kariorkor.
JIVU KWA JIVU: Uchomaji wa mwili wa aliyekuwa wakili wa serikali Satish Gautama katika makaburi ya Kariorkor.
Image: MAKTABA

TAARIFA YA GORDON OSEN 

Janga la Covid-19 limesababisha uhaba wa kuni katika chumba cha maiti cha Kariokor kwa watu wa jamii ya Asia na jamii hiyo inaomba misaada ya haraka ya kuni kavu.

Watu wa umri wa juu kutoka jamii ya Asia nchini wamekuwa miongoni mwa walioathirika zaidi na janga la Covid-19. Jamii hiyo kwa kawaida huteketeza miili ya wapendwa wao kuambatana na tamaduni zao.

 

Ombi hilo linakusudia kuhakikisha kuwa watu wengi wanaweza kuchoma miili ya wapendwa wao.

"Wiki iliyopita, tulitoa wito kwa watu wa jamii ya wahindi kutoa kuni kwani chumba chetu cha kuchomea miili  kinakabiliwa na uhaba wa kuni," mwanachama wa jamii ya Chuti alisema.

Msaidizi katika chumba cha kuchoma maiti, Harish Dariabhai, alisema kwamba mti wa blue gum hufanya vyema lakini kwa sasa kuni hizo zimeisha.

Amelazimika kutafuta msaada kutoka kwa marafiki ili kuafikia mahitaji.

Tanuri ya Kariakor ina uwezo kuteketeza miili minane hadi 10 kwa wakati mmoja lakini kwa sasa, ni miili miwili tu inayoweza kuchomwa kwa siku.

Uhaba wa kuni umeendelea kwa wiki mbili au tatu, lakini hali inazidi kuimarika kwani wahisani wanazidi kuitikia mwito na kuchanga kuni, "Dariabhai alisema.

Covid, hata hivyo, anaendelea kuangamiza  wahasiriwa zaidi.

 

"Zinahitajika haraka! Kwa sababu ya hali ya sasa ya Covid-19, vifo vingi vinatokea, kwa hivyo, tunahitaji sana magogo (kuni) kwa Shamsan Bhumi yetu.

"Ombi la unyenyekevu kwa wanachama wote kusaidia," rufaa kwenye mitandao ya kijamii ilisema.

"Ni muhimu sana. Jamaa mpendwa wa Wahindu, familia zinahitaji msaada wako. Tafadhali nisaidie na usambaze ujumbe huu kwa vikundi vingi iwezekanavyo."

Mbali na idadi kubwa ya vifo vya Covid-19 katika jamii, mhudumu huyo alisema, shinikizo zimezidi kwa sababu Kariokor ndicho kituo cha pekee kinachohudumia jamii ya Waasia ya Nairobi.

"Fikiria, katika Nairobi nzima, hapa ndipo mahali pekee pa kuchomea maiti panapowahudumia Waasia. Kwa hivyo shinikizo kutoka kwa idadi iliyoongezeka ni ya kweli," Dariabhai alisema.

Alisema amelazimika kutegemea marafiki kupata kuni za blue gum  zizokaushwa. Zile tuko nazo ni kwa sasa ni mbichi na inachukua muda mrefu kuchoma, licha ya mafuta yaliyoongezwa.

"Familia husika husubiri kwa muda mrefu kuchomeka kwa mwili wa mpendwa wao ili kubeba majivu kwenda nyumbani. Mbao mbichi hufanya mchakato huo kuwa wa kuchosha," Dariabhai alisema.