Kesi ya mauaji dhidi ya Jowie na Maribe kusikilizwa katika mahakama ya wazi

Muhtasari

• Katika vikao vya kusikiliza kesi hiyo vilivyopita, mahakama ilisikia kwamba mfanyabiashara huyo aliishi na mwanamume katika nyumba yake ya Lamuria.

Mwanahabari Jacque Maribe na Jowie Irungu katika mahakama ya Milimani Jumanne, Novemba 26, 2019.
Mwanahabari Jacque Maribe na Jowie Irungu katika mahakama ya Milimani Jumanne, Novemba 26, 2019.
Image: ENOS TECHE

Kesi ya mauaji inayowakabili Joseph Irungu kwa jina maarufu kama Jowie na mwanahabari Jacque Maribe kuhusiana na mauaji ya mfanyabiashara Monica Kimani itaendelea katika mahakama ya wazi mwezi Mei.

Kesi hiyo ilikuwa isikizwe siku ya Jumatano kwa njia ya video lakini iliahirishwa baada ya pande zote kutaka kesi hiyo isikilizwe katika mahakama ya wazi.

Jaji Grace Nzioka aliagiza kesi hiyo isikilizwe Mei 5 katika mahakama ya wazi.

 

Katika vikao vya kusikiliza kesi hiyo vilivyopita, mahakama ilisikia kwamba mfanyabiashara huyo aliishi na mwanamume katika nyumba yake ya Lamuria.

Mashahidi wanne akiwemo mtunza bustani, msimamizi wa ploti, mhudumu na rafiki wa Maribe walitoa ushahidi mbele ya Jaji James Wakiaga.

Wanne hao ambao ni mashahidi wa upande wa mashtaka walisema mfanyabiashara huyo aliishi na mtu aliyeitwa Yaseen. Alikuwa na umri wa miaka 24 wakati wa kifo chake.

Msimamizi wa bustani ya Lamuria Stephen Wanjohi alisema Yaseen alitembelea nyumba hiyo mwaka huu kukusanya mali zake.

Korti ilisikia kwamba Yaseen hakuwepo wakati wa mazishi ya Monica.

Mtunza bustani Regan Buluku alisimulia jinsi aliingia katika nyumba ya Monica kupitia balcony na alikuwa mtu wa kwanza kuuona mwili wake.

Buluku alisema mwili ulikuwa kwenye bafu, na alikumbuka kuona mishumaa karibu na bafu.

 

Mhudumu wa uwasilishaji Dennis Wanjala alisema alitumwa kuchukua kitu kutoka kwa Monica alipofika Uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta siku ya Jumatano aliokufa.

Shahidi wa nne, rafiki wa Maribe Chelang’at Ruto, alithibitisha kuwa na Maribe pamoja na Gavana wa Nairobi Mike Sonko usiku wa mauaji.

Waliachana tu saa kumi asubuhi wakati Jowie alichukua Maribe kutoka kwenye eneo la burudani walipokuwa.

Ripoti ya uchunguzi wa serikali iliyowasilishwa kortini wakati wa kesi mwaka 2019 ilimhusisha Jowie na eneo la uhalifu, nyumba ya Monica.

Miezi mitano tu na wiki mbili tangu kuanza kwa kesi hiyo, mchambuzi wa serikali Dkt Joseph Kimani aliwasilisha ripoti inayoonyesha matokeo ya sampuli 73 zilizochukuliwa kutoka eneo la uhalifu.

Kufikia sasa, mashahidi 20 wameshirikishwa katika kesi hiyo.

Jacque na Jowie wamekana madai ya kumuua Monica usiku wa Septemba 19 na Septemba 20, 2018. Wako nje kwa dhamana ya pesa taslimu ya Shilingi 2 milioni moja kila mmoja.