Tahadhari yatolewa kuhusu mafuriko Mandera, Marsabit na Wajir

Muhtasari

• Wakaazi katika maeneo yote yaliyotajwa wamepewa tahadhari ya kuwa macho kwa sababu mafuriko yanayoweza kutokea katika maeneo ambayo mvua kubwa haijapokelewa haswa katika maeneo ambayo yanajulikana kuwa njia za maji kutoka nchi jirani ya Ethiopia

MVUA KUBWA: A tuk tuk ikisukumwa ndani ya maji ya mafuriko
MVUA KUBWA: A tuk tuk ikisukumwa ndani ya maji ya mafuriko
Image: JOHN CHESOLI

Idara ya utabiri wa hali ya hewa imeonya kuhusu uwezekano wa kutokea kwa mafuriko katika maeneo ya mpaka wa Kenya na Ethiopia.

Katika tahadhari siku ya Jumatano, mkurugenzi wa huduma za hali ya hewa Stella Aura alisema mafuriko hayo ni kutokana na mvua kubwa ya zaidi ya 50mm / kwa saa 24 eneo la Nyanda za Juu za Ethiopia.

"Hii inaweza kusababisha mtiririko wa maji katika kaunti za Mandera, Marsabit na Wajir," Aura alisema na kuongeza kuwa hali hiyo inatarajiwa kuanzia leo hadi Mei 1.

 

"Wakaazi katika maeneo yote yaliyotajwa wamepewa tahadhari ya kuwa macho kwa sababu mafuriko yanayoweza kutokea katika maeneo ambayo mvua kubwa haijapokelewa haswa katika maeneo ambayo yanajulikana kuwa njia za maji kutoka nchi jirani ya Ethiopia," alisema.

Siku nne zilizopita, Mamlaka ya Bandari ya Kenya ilionya kuhusu Kimbunga cha "Jobo" ambacho kimebainika kuelekea Ukanda wa Pwani ya Afrika Mashariki.

Kimbunga Jobo kilitabiriwa kutua bandarini siku ya Jumapili lakini haikufanya hivyo.

Tahadhari ya Bandari ya Mombasa na Uchukuzi wa meli ilitolewa kwa kipindi cha Aprili 25-27, 2021, wakati ambapo Bandari na maeneo ya karibu yatapata hali mbaya ya hewa, mvua kubwa inayoambatana na upepo mkali.

Mamlaka ilishauri kwamba meli zote katika Bandari ziangalie kwa makini hali ya hewa mbaya na kuchukua kila hatua inayofaa ili kuhakikisha meli ziko imara dhidi ya upepo mkali.