Tanga tanga imesambaratika - Junet

Muhtasari

• “Namba hizi zinaweza kusababisha vitu vingine. Namba hizi zinaweza kumfanya mtu apoteze kazi. Hatutaki kwenda njia hiyo kwa sababu tunataka kuzingatia ujenzi wa amani na kuwaleta Wakenya pamoja, "Junet alisema.

TAARIFA YA MOSES ODHIAMBO 

Wabunge wanaounga mkono BBI wanasema kuwa idadi kubwa ya wabunge waliounga mkono muswada wa marekebisho ya katiba siku ya Alhamisi usiku ni ishara ya “kifo cha kundi la Tangatanga” linaloongozwa na Naibu Rais William Ruto.

Viongozi hao wanashikilia kuwa kura hiyo ambayo ilikwenda vizuri kuelekea usiku wa manane ilitupilia mbali madai kuwa mrengo wa Ruto una idadi kubwa ya wabunge."

 

Walisema kuwa Ruto anapaswa kuwa na wasiwasi kwasababu hana kura yoyote kutoka Nyanza, Pwani, na alifanya vibaya katika maeneo ambayo amedai kuwa na ufwasi mkubwa kama vile eneo la Kati.

Wabunge wanaounga mkono BBI walisema uungwaji mkono na wabunge 235 katika awamu ya tatu ya muswada huo inapaswa kuwapa wasiwasi maafisa wa serikali, ikiwa ni idadi inayohitajika kupitisha kura ya kutokuwa na imani na afisa mkuu wa serikali.

Kiongozi wa walio wengi katika Bunge la Kitaifa Amos Kimunya, kiranja wa Wachache Junet Mohamed, kiranja wa wengi Emmanuel Wangwe na naibu wake Maoka Maore, na katibu wa wabunge wa Jubilee Adan Keynan walizungumzia suala hilo.

“Jana, kulingana na mimi kulikuwa na kifo cha Tangatanga kisiasa. Chaguo lilikuwa kati ya toroli na ustawi; kati ya hiki kitu ‘bottom-up’ na umoja, ”Junet alisema.

Alisema umaarufu wa Naibu rais unazidi kudidimia kila siku na ikizingatiwa kwamba wabunge 83 walipiga kura kupinga katika duru ya kwanza na ni 63 tu waliopinga katika duru ya pili "lazima wafikiriye nini kimebadilika."

“Namba hizi zinaweza kusababisha vitu vingine. Namba hizi zinaweza kumfanya mtu apoteze kazi. Hatutaki kwenda njia hiyo kwa sababu tunataka kuzingatia ujenzi wa amani na kuwaleta Wakenya pamoja, "Junet alisema.

Mwenyekiti mwenza wa sekretarieti ya BBI Denis Waweru alisema sasa wanatarajia Seneti itahitimisha ili waandaye kura ya maoni.

 

"Kwa wale ambao walikuwa na shaka kuwa hakutakuwa na kura ya maoni katika nchi hii, jibu lilikuwa jana usiku," alisema.

"Tulikuwa tukitishwa na watu ambao wamekuwa wakidai kuwa wana idadi," Maore alisema.