KUDHIBITI KORONA SIAYA

Hakuna kupika wala kupiga sherehe mazishini huko Siaya!

Serikali ya kaunti ya Siaya yaweka mikakati mikali ili kujaribu kudhibiti ongezeko ya visa vya Korona.

Muhtasari

•Serikali ya kaunti ya Siaya yapiga marufuku kupika na kupiga sherehe kwenye mazishi.

• Asilimia ya maambukizi katika kaunti ya Siaya ni 26%.

gavana wa siaya
gavana wa siaya
Image: Hisani: The Star

Kutokana na ongezeko ya visa vya COVID 19 katika kaunti ya Siaya,serikali ya kaunti hiyo imemwandikia kamishna wa kaunti ikitaka utekelezaji wa dharura wa mikakati za kudhibiti kuenea kwa virusi hivyo.

Mkutano uliofanyika siku ya Ijumaa kujadili mipango ya kudhibiti virusi vya Korona uliafikia hatua kali zichukuliwe.

Kati ya mikakati iliyowekwa ni kupiga marufuku kupika au kupiga sherehe kwenye mazishi, miili ya wafu kuzikwa ndani ya masaa 48 baada ya kifo, mikutano ya kamati ya kujadili mikakati ya kukabiliana na virusi vya Korona kurejeshwa na kuteuliwa kwa timu ya kufuatilia utekelezaji wa mikakati iliyowekwa haswa kwenye mazishi, nyumba za ibada, sokoni, kwenye magari na kwenye nyumba za kuhifadhi maiti.

Kwa sasa asilimia ya maambukizi katika kaunti hiyo imesimia 26%.