Sababu za mwanamke kujifungua watoto wengi kwa pamoja

Muhtasari

• Wataalamu wanasema kuwa na mimba ya watoto wengi kwa mara moja hutokea iwapo tu kama mtu ametumia tiba ya uzazi.

• Baada ya kusubiri kwa takribani miaka saba bila mtoto, Joyce Akhimien alijifungua watoto mapacha sita.

 

Image: AFRICAN NEWS AGENCY (ANA)

Mwanamke wa Afrika Kusini , Gosiame Thamara Sithole amejifungua watoto 10 na kuvunja rekodi ya kuzaa watoto wengi.

Mara nyingi huwa ni matokeo ya kufanya tiba ya uzazi - lakini wapenzi hawa wanasema wao walitumia njia ya asili kupata mimba.

Teboho Tsotetsi, mume wa mwanamke huyo mwenye miaka 37 anasema kuzaliwa kwa watoto kumi ni jambo ambalo hawakulitegemea kwa kuwa waliona watoto nane tu walipopiga picha wakati wa ujauzito.

Wataalamu wanasema kuwa na mimba ya watoto wengi kwa mara moja hutokea iwapo tu kama mtu ametumia tiba ya uzazi.

Mwezi uliopita , Halima Cissé mwenye miaka 25 kutoka Mali alijifungua watoto tisa kwa mara moja ,na walikuwa wanaendelea vyema wote katika kliniki moja iliyopo Morocco.

Deaconess Doris Levi Wilson mwenye umri wa miaka 49 alipata watoto wasichana wanne na wavulana wawili Februari, 9, 2021.
Deaconess Doris Levi Wilson mwenye umri wa miaka 49 alipata watoto wasichana wanne na wavulana wawili Februari, 9, 2021.

Baada ya kusubiri kwa takribani miaka saba bila mtoto, Joyce Akhimien alijifungua watoto mapacha sita : watoto wavulana wanne na watoto wasichana wawili tarehe 12 Januari, 2021 huko Port Harcourt, Nigeria.

Hali ilikuwa vivyo hivyo kwa Doris Wilson mwenye miaka 49 yeye alisubiri miaka 21 na siku alipopata watoto Februari, 9 maka huu alipata watoto sita huko Nigeria.

Mimba nyingi zinazopelekea watu kujifungua watoto wengi , watoto wake huwa wanazaliwa kabla ya siku zao.

Sababu zinazopelekea mwanamke kuwa na mimba ya watoto wengi?

Si jambo la kawaida kwa mwanamke kuzaa watoto zaidi ya watatu.

Lakini mtaalamu wa masuala ya afya ya uzazi Bill Kalumi, kutoka hospitali ya taifa ya Kenya imesema:

"Mara nyingi hali hii hutokea iwapo mtu ametumia tiba ya uzazi."

Ingawa kuna sababu inayowafanya watu kutafuta tiba ya uzazi.

Joyce Akhimien, 39 ni mama aliyepata watoto wengi kwa wakati mmoja
Joyce Akhimien, 39 ni mama aliyepata watoto wengi kwa wakati mmoja

Lakini hali hii hutokea sana barani Afrika wakati ambao mwanamke anaanza kutumia dawa za homoni ambazo ni kama za kuzuia kupata ujauzito.

Hii inaweza kumchukua muda kwa kipindi cha kutungwa mimba, Dkt Kalumi anaeleza.

Hivyo matokeo yake yanaweza kuwa mayai mengi badala ya moja wakati wa mzunguko wa mwanamke kwa mwezi.

Uzazi wa watoto wengi kwa pamoja, ni jambo la hatari kwa mama na watoto.

Mara nyingine baada ya kufanya vipimo vya picha, inashauriwa kupunguza idadi ya watoto waliopo tumboni.

Si rahisi kuwatunza watoto wengi kwa pamoja
Si rahisi kuwatunza watoto wengi kwa pamoja
Image: EPA

Na watoto wanaozaliwa kabla ya muda wao yani kabla ya wiki 37, wako kwenye hatari ya kupata matatizo.

Watoto kuzaliwa wengi wako kwenye hatari ya kupata maambukizi.

Kwa muda mrefu watoto wanapozaliwa wengi, wanaweza kupata matatizo ya afya ambayo inaweza kusababisha matatizo ya kutembea.

Kwa huyu mama aliyejifungua watoto 10 hivi karibuni, Daktari anasema Sithole yupo kwenye hali nzuri.

Image: AFRICAN NEWS AGENCY (ANA)

Gosiame Thamara Sithole alijifungua kwa njia ya upasuaji wakati mimba ikiwa na wiki 29 , huko Pretoria Jumatatu jioni.

Katika kitabu cha maajabu ya ulimwengu , Guiness ambapo wamesema wanafanya utafiti juu ya kesi ya bi Sithole .

Mwanamke aliyejifungua watoto nane mwaka 2009 huko Marekani ndio anashikilia rekodi ya dunia ya Guiness kwa kujifungua watoto wengi kwa pamoja na wote kupona.

Dawa za kisasa tayari zinaruhusu wanawake kujifungua watoto umri ukiwa umeenda tofauti na wakati wa mababu zetu.