Uporaji ulisheheni serikali yangu katika muhula wa kwanza - Uhuru

Muhtasari

• Uhuru aliwaambia viongozi kuwa ameweza kusajili mafanikio makubwa katika utendakazi wake katika muhula wa pili kwa sababu aliwaacha 'wezi' na kukubali umoja.

• Rais alizungumzia jinsi viongozi wengine walijitajirisha wakati wa kipindi chake cha kwanza.

Ahadi zilizovunjwa
Ahadi zilizovunjwa

TAARIFA YA JAMES MBAKA

Rais Uhuru Kenyatta na Naibu Rais William Ruto wanaelekea kwenye vita vikali vya kisiasa baada ya rais kusema kwamba muhula wake wa kwanza ulitikiswa na ufisadi mkubwa.

Ingawa Rais hakumtaja Ruto, ilikuwa wakati wa mkutano na viongozi wa Ukambani kwamba alitangaza atamuunga mkono mgombea wa Nasa kumrithi, akimwondoa Ruto kutoka hesabu zake za urithi.

Ruto amesukumwa pembezoni mwa uendeshaji wa serikali tangu ‘handshake’ ifanyike Machi 9, 2018 kati ya Rais Uhuru na kinara wa Upinzani Raila Odinga.

Usemi wa Uhuru siku ya Jumatatu unaweza kuwa ulimlenga Ruto, ambaye alikuwa nguzo muhimu katika usimamizi wa maswala ya serikali katika kipindi chao cha kwanza kati ya 2013 na 2017.

Tangazo la Uhuru kwamba atamuunga mkono mmoja katika muungano wa Nasa kuwa urais mwaka ujao lilionekana kumkwaza roho, naye akazamia mtandao wa Twitter kukashifu na kukejeli usemi huo wa rais.

Alimshtumu rais kwa usaliti na akafanya ishara rasmi kwamba anaweza kuwa njiani kuondoka chama tawala cha  Jubilee.

Tangazo la Uhuru kwamba atachagua mrithi wake wa 2022 kutoka viongozi wa Nasa ikiwa wataungana na kukubaliana kuwa mgombeaji mmoja liliripotiwa na gazeti la The Star siku ya Jumanne.

“Kwa hivyo! Uharibifu / kusambaratishwa kwa Jubilee, chama cha kitaifa, kulilenga kufungua njia ya kuungwa mkono na vyama vya kikanda / kabila huko Nasa? Na sasa, vile Jubilee imesambaratika, si  sawa kwa wale ambao hawawezi kutoshea katika vyama vya kikabila kujenga UDA kama chama mbadala cha kitaifa? Ama? ” Ruto alituma tweet pamoja na picha za taarifa ya Star.

Mapema siku hiyo, DP alikuwa amehoji busara ya Uhuru kuunga mkono upinzani, na ilhali kulikuwa na Wakenya milioni nane ambao walipigia kura chama tawala katika chaguzi tatu.

“Hakuna, hakuna kijana, hakuna mwanamke, hakuna mtu katika ya milioni M ambaye aliamka mapema na kupiga kura mara 3 kwa tikiti ya UK/ WsR? Ni sawa. Tutapanga kwa msaada wa Mungu, "alisema.

Ruto mnamo Februari alisema hakuna mtu anayemdai chochote na kwamba hakuunga mkono Uhuru kwa kazi hiyo ili pia apate kuungwa mkono. Hahitaji kuidhinishwa na mtu yeyote kutafuta urais, Ruto alisema.

Maelezo yaliyopatikana kutoka kwa viongozi wa Ukambani ambao walihudhuria mkutano katika Ikulu siku ya Jumatatu Rais alizungumzia jinsi viongozi wengine walijitajirisha wakati wa kipindi chake cha kwanza.

Uhuru aliwaambia viongozi hao kuwa sasa ameweza kusajili mafanikio makubwa katika utendakazi wake katika muhula wa pili kwa sababu aliwaacha 'wezi' na kukubali umoja.

"Rais alitupitisha katika kipindi chake cha kwanza na kusema waziwazi kuwa watu wengine waliiba fedha za umma na wakawa mabilionea usiku kucha lakini hawawezi kuelezea jinsi walivyopata utajiri wao," mbunge wa Ukambani aliyehudhuria mkutano alisema.

(Imetafsiriwa na kuhaririwa na Davis Ojiambo)