Watu 796 waambukizwa Covid-19, watatu waaga

Jumla ya wagonjwa 328 wamepona ugonjwa huo, 307 wakiwa chini ya uangalizi wakiwa nyumbani kwao huku 21 wakipona kutoka hospitalini

Muhtasari

• Kufikia sasa Kenya sasa imesajili jumla ya visa 178,078 vya maambukizi ya Covid-19.

• Jumla ya wagonjwa 1,097 kwa sasa wamelazwa hospitalini, wengine 4,842 wako chini ya uangalizi nyumbani.

Watu watatu zaidi wamefariki kutokana na maambukizi ya vitusi vya Covid-19, huku watu wengine 796 wakiambukizwa kutoka kwa sampuli 7,392 katika takwimu mpya zilizotangazwa na wizara afya chini ya saa 24 zilizopita. Kiwango cha maambukizi sasa kimetimia asilimia 10.8.

Kufikia sasa Kenya sasa imesajili jumla ya visa 178,078 vya maambukizi ya Covid-19.

Kutoka kwa visa vipya , 746 ni rais wa Kenya huku watu 50 wakiwa raia wa kigeni.

Jumla ya wagonjwa 328 wamepona ugonjwa huo, 307 wakiwa chini ya uangalizi wakiwa nyumbani kwao huku 21 wakipona kutoka hospitalini.

Jumla ya watu 122,346 waliokuwa wameambukizwa virusi hivyo nchini wamepona.

Wizara pia ilitangaza vifo vya watu watatu, vyote kufikisha idadi ya watu 3,437 waliofariki nchini.

Jumla ya wagonjwa 1,097 kwa sasa wamelazwa hospitalini, wengine 4,842 wako chini ya uangalizi nyumbani.

Wagonjwa wengine 89 wako kwenye vyumba vya wagonjwa mahututi, 26 kati yao wamewekwa kwenye mashine za kuwawezesha kupumua  na 49 kwenye oksijeni ya kuongezea, huku 14 wakiwa chini ya uangalizi.

Wagonjwa wengine 114 wako kwa oksijeni ya ziada, 109 kati yao katika wodi za jumla na lakini watano wako katika kitengo cha HDU.

Visa hivi vipya vimesambaa katika kaunti mbali kama ifuatavyo; Nairobi 174, Siaya 138, Kisumu 92, Bomet 62, Mombasa 46, Busia 41, Homa Bay 30, Kisii na Uasin Gishu visa 24 kila moja, Vihiga 23, Kakamega 19, Nakuru 16, Trans Nzoia 15, Bungoma 13, Kilifi 11, Kiambu tisa, Kajiado, Kericho na Meru visa vinane kila moja, Nandi sita, Garissa na Kwale vinne kila mmoja na Migori tatu.

Lamu, Murang’a, Nyandarua, Nyeri, Taita Taveta, Turkana na Pokot Magharibi zina visa viwili kila moja, huku Elgeyo Marakwet, Laikipia, Machakos na Narok zikirekodi kisa kila moja.