Al Shabaab: Mshukiwa mmoja auliwa, 2 watoroka na majeraha walipovamiwa wakipanga njama ya kigaidi Kwale

Bunduki aina ya AK47, risasi 763 na karatasi iliyokuwa imeandikwa maeneo ambayo yalikuwa yanalengwa ni baadhi ya vitu vilivyopatikana

Muhtasari

•Watatu hao walikuwa mafichoni wakati maafisa waliokuwa wanawatafuta waliwapata hatimaye na kuwapiga risasi.

•Mmoja wao anaripotiwa kujeruhiwa vibaya hadi kuaga huku wenzake wawili wakiweza kutoroka na majeraha kadhaa ya risasi mwilini.

crime scene
crime scene

Maafisa wa polisi walivizia watu watatu walioshukiwa kuwa wanamgambo wa Alshabaab na kuua mmoja huku wawili wengine wakitoweka na majeraha ya risasi katika maeneo ya Bombo, Kwale.

Ripoti iliyochapishwa na maafisa wa DCI inaashiria kuwa watatu hao walivamiwa wakati walikuwa wanapanga njama ya kufanya mashambulizi katika maeneo hayo ya Kwale

Watatu hao walikuwa mafichoni wakati maafisa waliokuwa wanawatafuta waliwapata hatimaye na kuwapiga risasi.

Mmoja wao anaripotiwa kujeruhiwa vibaya hadi kuaga huku wenzake wawili wakiweza kutoroka na majeraha kadhaa ya risasi mwilini.

Bunduki aina ya AK47, risasi 763  na karatasi iliyokuwa imeandikwa maeneo ambayo yalikuwa yanalengwa baadhi ya vitu ambavyo vilipatikana katika eneo la tukio.

Kipakatalishi aina ya HP, simu tisa, redio ya kucheza muziki miongoni mwa bidhaa zingine pia zilipatikana pale .

Mwili wa mshukiwa aliyeuliwa ulipelekwa katika mochari ya hospitali ya Kwale huku maafisa wa kupambana na ugaidi wakiendelea kufanya upelelezi zaidi kuhusiana na tukio hilo.