ALISHTAKIWA PAMOJA NA WENGINE 5

Mkenya akubali mashtaka ya ulaghai wa kimapenzi unaohusisha zaidi ya Sh430,000,000 huko Marekani

Inadaiwa kuwa Mwende pamoja na wengine walijipatia utambulisho bandia mitandaoni ili kuvutia hisia za kimapenzi na uaminifu kutoka kwa wahairiwa

Muhtasari

•Mwende ambaye alikuwa akiishi jijini Canton, Ohio  pamoja na wenzake wanadaiwa kulaghai kikundi kikubwa cha watu mitandaoni zaidi ya Ksh430,000,000. 

•Sheria za Marekani zinapendekeza kifungo cha miaka 30 au faini ya Sh107, 300,000 na kufuatiliwa kwa karibu baada ya kuachiliwa ama kulipa mara mbili kiwango cha pesa ambacho washukiwa wanadaiwa kuiba, kwa kesi hii ikiwa zaidi ya Sh860,000,000.

court
court

Huenda raia mmoja wa Kenya anayeishi Marekani akahudumu kifungo cha takriban miaka 30 baada ya kukubali mashtaka ya kuhusika kwenye ulaghai wa kimapenzi.

Florence Mwende Masau, 36,alikubali shtaka la kuhusika kwenye ulaghai ambapo walipokea pesa kutoka kwa watu ambao walianguka kwenye mtego wa mapenzi bandia. Hata hivyo,   washukiwa wengine watano walioshtakiwa pamoja naye walikanusha mashtaka.

Mwende ambaye alikuwa akiishi jijini Canton, Ohio  pamoja na wenzake wanadaiwa kulaghai kikundi kikubwa cha watu mitandaoni zaidi ya Ksh430,000,000. 

Karatasi ya mashtaka ilidai kuwa Mwende alihuskia katika ulaghai wa kimitandao ambapo waliibia walishawishi watu kutuma pesa kwenye akaunti ya benki ambayo alimiliki pamoja na wengine.

Inadaiwa kuwa Mwende pamoja na wenzake walijipatia utambulisho bandia mitandaoni ili kuvutia hisia za kimapenzi na uaminifu kutoka kwa watu.

Wangejifanya kuwa  na uhusiano wa kimapenzi wa karibu na wahasiriwa ili kuwashawishi kutuma pesa.

Ili kutekeleza hayo, Musau anaripotiwa kutumia pasipoti bandia zilizoandikishwa kwa majina mengi bandia ili kufungua akaunti za benki tofauti jijini Boston na viunga vyake. Akaunti hizo zilitumika kupokea pesa ambazo walipata kutoka kwa watu waliokuwa wameanguka kwenye mtego wa mapenzi bandia.

Sheria za Marekani zinapendekeza kifungo cha miaka 30 au faini ya Sh107, 300,000 na kufuatiliwa kwa karibu baada ya kuachiliwa ama kulipa mara mbili kiwango cha pesa ambacho washukiwa wanadaiwa kuiba, kwa kesi hii ikiwa zaidi ya Sh860,000,000.

Hukumu ya Mwende itatolewa na jaji Allison D. Burroughs  mnamo Oktoba 14, 2021.