(+Picha) Rais Kenyatta, Ruto na Raila waketi kwa jukwaa moja wakati wa maadhimisho ya Mashujaa Day

Muhtasari

•Rais Uhuru Kenyatta, naibu rais William Ruto na kinara wa ODM Raila Odinga waliketi katika jukwaa moja wakati Kenya ilikuwa inasherehekea maadhimisho ya 58 ya siku ya Mashujaa.

Rais Kenyatta na naibu rais William Ruto wakisalimiana wakati wa maadhimisho ya siku ya Mashujaa
Rais Kenyatta na naibu rais William Ruto wakisalimiana wakati wa maadhimisho ya siku ya Mashujaa
Image: MERCY MUMO

Kaunti ya Kirinyaga ilikaribisha vigogo watatu wakuu wa siasa nchini wakati wa maadhimisho ya siku ya Mashujaa yaliyofanyika katika uwanja wa Wang'uru siku ya Jumanne.

Rais Uhuru Kenyatta, naibu rais William Ruto na kinara wa ODM Raila Odinga waliketi katika jukwaa moja wakati Kenya ilikuwa inasherehekea maadhimisho ya 58 ya siku ya Mashujaa.

Rais Kenyatta na Ruto wasalimiana
Rais Kenyatta na Ruto wasalimiana
Image: MERCY MUMO

Ruto hawajaonana jicho kwa jicho na rais Kenyatta tangu tarehe 1 mwezi Juni wakati wa maadhimisho ya siku ya Madaraka yaliyofanyika kaunti ya Kisumu.

Hivi majuzi Ruto alisema kwamba alisaidia Uhuru na Raila kupata  uongozi ila wakaungana pamoja kumpinga.

Mnamo Agosti 23, Uhuru aliambia Ruto hadharani ajiuzuru kutoka serikalini iwapo hajaridhishwa na namna kazi imekuwa ikitekelezwa badala ya kumkosoa akiwa serikalini.

Rais Kenyatta na DP Ruto
Rais Kenyatta na DP Ruto
Image: MERCY MUMO

Naibu rais aliwasili mida ya saa tano asubuhi na kushangiliwa sana na watu kabla ya kuenda kusalimia waheshimiwa wengine ikiwemo Raila Odinga, Musalia Mudavadi, Gideon Moi kati ya wengine.

Baadae alienda kumkaribisha rais wa Malawi Lazarus Chakwera ambaye alikuwa mgeni mkuu katika maadhimisho ya siku ya Mashujaa mwaka huu.

Rais aliwasili baadae mida ya saa tano unusu na akazungushwa uwanjani huku akisalimia watu waliokuwa wamejumuika kabla ya kukaguwa gwaride la heshima lililojumuisha wanajeshi wa KDF.

Raila Odinga asalimia Gideon Moi na Moses Wetangula
Raila Odinga asalimia Gideon Moi na Moses Wetangula
Image: MERCY MUMO

Viongozi wengine ambao walihudhuria hafla hiyo ni pamoja na kiongozi wa ANC Musalia Mudavadi, Kiongozi wa KANU Gideon Moi, Kiongozi wa Narc-Kenya Martha Karua na Jaji Mkuu Martha Koome.

Wengine ni pamoja na wabunge kutoka kaunti ya Kirinyaga, maseneta mbalimbali, spika wa bunge la kitaifa Justin Muturi na wa seneti Kenneth Lusaka, waziri Najib Balala, Farida Karoney na Fred Matiang'i.

Rais Kenyatta akikagua gwaride la heshima
Rais Kenyatta akikagua gwaride la heshima
Image: MERCY MUMO

Magavana ambao walihudhuria ni pamoja na Ann Waiguru wa Kirinyaga, Hassan Joho wa Mombasa, Mwangi wa Iria wa Murang'a, Martin Wambora wa Embu, Mutahi Kahiga wa Nyeri, Nderitu Muriithi wa Laikipia na Anyang' Nyong'o wa Kisumu.

(Utafsiri: Samuel Maina)