Wanafunzi sita wa kike washtakiwa kwa kujaribu kuteketeza bweni Kiminini

Muhtasari

•Walipofikishwa mbele ya Hakimu Mkuu wa mahakama  Kitale Mary Achieng alasiri ya Alhamisi wanafunzi hao walishtakiwa kwa kushirikiana kutekeleza uhalifu.

•Wanafunzi hao walikuwa wamenunua nusu lita ya mafuta ya taa, kilo moja ya chumvi na sanduku la kiberiti ambalo walikusudia kutumia kuchoma bweni lao lililopewa jina la St. Ann's Storey.

court
court

Wanafunzi sita wa kidato katika Shule ya Upili ya Wasichana ya St. John’s, Sirende katika Kaunti Ndogo ya Kiminini wameshtakiwa kwa kujaribu kuteketeza bweni.

Walipofikishwa mbele ya Hakimu Mkuu wa mahakama  Kitale Mary Achieng alasiri ya Alhamisi wanafunzi hao walishtakiwa kwa kushirikiana kutekeleza uhalifu.

 Kulingana na karatasi ya mashtaka, sita hao walishtakiwa kwa kujaribu kuchoma bweni katika shule yao mnamo tarehe 3 Novemba, 2021 kinyume na kanuni ya adhabu.

 Hata hivyo, wanafunzi hao sita walikanusha mashtaka waliyoandikishwa na kuzuiliwa katika kituo cha polisi cha Kitale.

Mahakama pia iliamuru wapelekwe katika Hospitali ya Rufaa ya Kaunti ya Kitale kwa uchunguzi wa kidaktari pamoja na kutathminiwa umri.

Kesi hiyo itatajwa Novemba 9, 2021.

 Akizungumza na KNA Mkuu wa shule hiyo Linet  Ooko alisema kuwa amepata taarifa muhimu kutoka kwa Kasisi wa taasisi hiyo ambaye aliwaona wasichana hao wakinunua mafuta ya taa katika kituo cha ununuzi cha Sirende mnamo Jumatano 7:45pm.

 "Tulipiga simu bila kukusudia na hakika wanafunzi hao sita kutoka kidato cha pili Mashariki hawakupatikana na baada ya msako wa haraka, walipatikana wamejificha katika choo kimoja," alifichua Ooko, akiongeza baada ya kuhojiwa wahalifu hao walikiri kutoroka kutoka shuleni.

Wanafunzi hao walikuwa wamenunua nusu lita ya mafuta ya taa, kilo moja ya chumvi na sanduku la kiberiti ambalo walikusudia kutumia kuchoma bweni lao lililopewa jina la St. Ann's Storey.

Ofisi za polisi kutoka kituo cha Kitale zilipata vitu vyote vilivyotajwa ambavyo vimehifadhiwa kama vielelezo vya mahakama.

(Utafsiri: Samuel Maina)