Heroin iliyokuwa imefichwa ndani ya vibuyu yapatikana JKIA

Muhtasari

•Wapelelezi wa kupambana na dawa za kulevya walikuwa wamepokea ripoti  kuhusu shehena ya kutiliwa shaka iliyokuwa imedaiwa kuwa vibuyu vya kiafrika (African Calabash) na ambayo ilikuwa tayari kusafirishwa kuelekea Canada

Ndege katika uwanja wa JKIA
Ndege katika uwanja wa JKIA
Image: DOUGLAS OKIDDY

Wapelelezi wa DCI jijini Nairobi wanasaka wafanyibiashara haramu ambao walikuwa wanajaribu kusafirisha Heroin hadi Canada.

Gramu 630 za mihadarati hiyo iliyokuwa imefichwa kwa vibuyu ilipatikana katika uwanja wa ndege wa JKIA siku ya Jumanne.

Wapelelezi wa kupambana na dawa za kulevya walikuwa wamepokea ripoti kutoka kwa walinzi wa DHL  kuhusu shehena ya kutiliwa shaka iliyokuwa imedaiwa kuwa vibuyu vya kiafrika (African Calabash) na ambayo ilikuwa tayari kusafirishwa kuelekea Canada wakati walifika katika uwanja wa ndege na kupata madawa hayo.

Uchunguzi ulibaini kuwa kweli kilichokuwa kwa vibuyu vile kilikuwa ni Heroini.

Kufuatia hayo msako wa mwenye shehena hiyo uling'oa nanga huku madawa yaliyopatikana yakuzuiliwa katika kituo cha polisi ili kutumika kama ushahidi.