WHO yaonya juu ya 'hatari kubwa ya maambukizi' ya Omicron kote ulimwenguni

Muhtasari

•Aina hiyo ya kirusi iligunduliwa nchini Afrika Kusini mapema mwezi huu huku ushahidi wa awali ukionyesha kuwa ina hatari kubwa ya maambukizo.

Image: GETTY IMAGES

Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) limeonya kuwa aina mpya ya kirusi cha corona Omicron kina hatari kubwa ya maambukizo kuongezeka kote ulimwenguni.

Aina hiyo inaweza kusababisha athari mbaya katika baadhi ya maeneo ya dunia , WHO ilisema Jumatatu.

Mkuu wa shirika hilo, Dk Tedros Adhanom Ghebreyesus, alitoa wito upya wa kushinikiza jamii ya kimataifa kutoa chanjo kwa mataifa maskini.

Covid-19 "hajamalizana nasi" bado, alionya.

Aina hiyo ya kirusi iligunduliwa nchini Afrika Kusini mapema mwezi huu huku ushahidi wa awali ukionyesha kuwa ina hatari kubwa ya maambukizo. Afrika Kusini imesifiwa kwa kuripoti kwa haraka kirusi hicho.

"Omicron ina idadi isiyokuwa ya kawaida ya mabadiliko ambayo mengine yanaweza kuwa athari kubwa katika mwelekeo mwingine wa janga," WHO ilisema.

Akizungumza Jumatatu, Dk Tedros alisema wanasayansi kote ulimwenguni wanafanya kazi ili kugundua ikiwa aina hiyo mpya inahusishwa na maambukizi ya juu, hatari ya kuambukizwa tena na jinsi inavyoitikia chanjo.

"Dharura ya Omicron ni ukumbusho mwingine kwamba ingawa wengi wetu tunafikiria kuwa tumemaliza Covid-19, janga hilo halijamalizana na sisi," alisema.

Aliongeza kuwa hakuna vifo ambavyo vimehusishwa na aina hiyo mpya ya kirusi cha Covid.

Visa tayari vimeripotiwa katika nchi kadhaa zikiwemo Canada, Uingereza, Ureno, Ubelgiji na Uholanzi.

Omicron imesababisha Uingereza, EU na Marekani kutoa marufuku ya kusafiri kwa nchi za Kusini mwa Afrika - uamuzi ulioshutumiwa na Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa.

Japan imetangaza kufunga mipaka yake kwa wageni wapya kutoka usiku wa Jumanne, wakati Australia imesitisha mpango wake uliosubiriwa kwa muda mrefu wa kupunguza vizuizi vya mipaka.

Kusafiri hadi Australia kwa wanafunzi wa kimataifa na "wafanyakazi wenye ujuzi" wanaoshikilia visa kulikusudiwa kuanza tena Jumatano lakini sasa kumeahirishwa hadi 15 Desemba.

Israel pia imepiga marufuku wageni kuingia nchini humo.

Image: BBC

Huko Uingereza, chanjo za ziada za Covid zinatarajiwa kutolewa kwa watu walio na umri wa zaidi ya miaka 18 ili kusaidia kusimamisha wimbi jipya linaloendeshwa na Omicron.

Marekani pia imefuata mkondo huku rais Joe Biden akiwaambia Wamarekani "nendeni mkachukue nyongeza ya chanjo ". Pia aliwataka watu kuvaa barakoa ndani ya nyumba.

Lakini Bw Biden pia alisema hatarajii vizuizi vyovyote.

Image: BBC

yote vya kusafiri vya Amerika au marufuku ya kutoka nje wakati huu.

Kumekuwa na visa zaidi ya milioni 261 na vifo milioni tano kote ulimwenguni tangu janga hilo lilipoanza mnamo 2020, kulingana na data kutoka Chuo Kikuu cha Johns Hopkins.