Mfanyibiashara anayesakwa kwa ukwepaji ushuru wa bilioni 2.2 atoroka mtego wa polisi - Weston

Polisi waliizingira hoteli hiyo huku msako dhidi ya wawili hao ukizidishwa bila mafanikio

Muhtasari

Kulikuwa na kizaazaa katika hoteli hiyo wakati polisi walipovamia hoteli hiyo kumsaka mwanamke huyo na mshukiwa mwenzake.

Inadaiwa walitumia mlango wa kuunganisha kutoka chumba chao cha ghorofa ya tatu kutorokea chumba cha pili na hivyo kufanya iwe vigumu kwa maafisa hao kuwafuatilia zaidi. 

Polisi waliizingira hoteli hiyo huku msako dhidi ya wawili hao ukizidishwa bila mafanikio.

Mfanyabiashara Mary Wambui. Picha: KWA HISANI
Mfanyabiashara Mary Wambui. Picha: KWA HISANI

Mfanyibiashara anayesakwa Mary Wambui Mungai, ambaye anasakwa kuhusiana na madai ya ukwepaji ushuru wa Shilingi bilioni 2.2 sikuya Jumatano usiku alikwepa mtengo wa polisi katika hoteli ya Weston, Nairobi ambako amekuwa akiishi. 

Kulikuwa na kizaazaa katika hoteli hiyo wakati polisi walipovamia hoteli hiyo kumsaka mwanamke huyo na mshukiwa mwenzake ndipo walipogundua kwamba alikuwa ameondoka muda mfupi uliyokuwa umepita na kuacha bidhaa zao za kibinafsi. 

Baadhi ya watu mashuhuri kutoka Garissa walikuwa katika eneo kwa ajili ya kuchangisha pesa. Naibu Rais William Ruto alikuwa miongoni mwa waliokuwa wakihudhuria. 

Haijabainika iwapo Naibu rais alifahamishwa kuhusu tukio hilo wakati polisi wakiwasaka wawili hao wakitumia agizo la mahakama. 

Mamlaka ya ukusanyaji Ushuru nchini Kenya (KRA) katika taarifa ilisema Wambui, pamoja na Purity Njoki Mungai, ambao wote ni wakurugenzi wa Purma Holdings Limited, walitoroka kutoka vyumba vyao vya hoteli dakika chache kabla ya polisi na maafisa wa KRA kufika kuwakamata. 

"Walipopekua katika majengo ya hoteli hiyo, maafisa wa KRA na polisi walipata vifaa vya kibinafsi vya wawili hao ikiwa ni pamoja na pesa taslimu, kadi za benki na funguo za gari, jambo linaloonyesha wazi kwamba wawili hao walikuwa wakiishi katika hoteli hiyo," KRA ilisema. 

Inadaiwa walitumia mlango wa kuunganisha kutoka chumba chao cha ghorofa ya tatu kutorokea chumba cha pili na hivyo kufanya iwe vigumu kwa maafisa hao kuwafuatilia zaidi. 

Polisi waliizingira hoteli hiyo huku msako dhidi ya wawili hao ukizidishwa bila mafanikio.Wageni waliokuwa hotelini waliondoka.