DP Ruto ajivunia matokeo ya chaguzi ndogo za Kiagu na Mahoo

Muhtasari

Kulingana na matokeo yaliyotangazwa na Tume Huru ya uchaguzi (IEBC), UDA ilifanikiwa kutwaa ushindi katika wadi ya Kiagu kaunti ya Meru huku ikiibuka ya pili katika wadi ya Mahoo.

Viongozi mbali mbali  wa Hustler Nation hawajaficha furaha yao kufuatia ushindi huo kupitia mitandao ya kijamii huku wakiwapongeza washindi na kujivunia ungwaji mkono wa juu .

Naibu Rais William Ruto
Naibu Rais William Ruto
Image: HISANI

Chama kinachohusishwa na Naibu wa Rais William Ruto cha UDA kimeonyesha ubabe katika chaguzi  ndogo zilizoandaliwa siku ya Alhamisi.

Kulingana na matokeo yaliyotangazwa na Tume Huru ya uchaguzi (IEBC), UDA ilifanikiwa kutwaa ushindi katika wadi ya Kiagu kaunti ya Meru huku ikiibuka ya pili katika wadi ya Mahoo.

Simon Kiambi ambaye alipeperusha bendera ya  UDA huko  Kiagu alipata ushindi baada ya kunyakua kura 2,440 huku Daniel  Kimuyu aliyewakilisha UDA Mahoo akiibuka wa pili kwa kura 1358.

Aliyeibuka mshindi kwenye wadi ya Mahoo  alikuwa Donald Fundi wa Jubilee akiwa na kura 1,609 akifuatwa kwa ukaribu na Kimuyu kwa  kura  1358 huku watatu akiwa ni Obwage Samuel wa chama cha Tujibebe Wakenya Party. 

Viongozi mbali mbali  wa Hustler Nation hawajaficha furaha yao kufuatia ushindi huo kupitia mitandao ya kijamii huku wakiwapongeza washindi na kujivunia ungwaji mkono wa juu .

Ruto kupitia mtandao wake wa twitter amenakili  “Wananchi wa wadi za Kiagu na Mahoo kaunti ya Meru na Taita Taveta wameipa ajenda ya kiuchumi ya Hustler Nation. Wamesema ndio kwa chama chao cha kitaifa”

Isitoshe Ruto hakusahau kuwapongeza viongozi hao waliopeperusha bendera ya Hustler Nation.

“Hongera Mheshimiwa  Simon Kiambi kwa kushinda katika Kiagu na Mheshimiwa  Daniel Kimuyu kwa kushika nafasi ya pili katika Mahoo. Taifa la Hustler lina nguvu