(+PICHA)Dennis Itumbi apatikana amepigwa kikatili muda mfupi baada ya kudaiwa kutekwa nyara

Muhtasari
  • Dennis Itumbi apatikana amepigwa kikatili muda mfupi baada ya kudaiwa kutekwa nyara
Dennis Itumbi apatikana amepigwa kikatili muda mfupi baada ya kudaiwa kutekwa nyara
Image: Kipchumba Murkomen/TWITTER

Mwanablogu na mshirika wa karibu wa DP William Ruto Dennis Itumbi amepatikana akiwa hai baada ya kudaiwa kutekwa nyara jana (Alhamisi) alipokuwa akitoka kwenye kinyozi.

Ripoti kwenye mitandao ya kijamii zilifichua kuwa Itumbi alitekwa nyara na kuwekwa ndani ya gari ambalo lilitoweka bila kujulikana.

Kulikuwa na madai kuwa alikamatwa kwa kukosa kuheshimu wito wa mahakama kuhusu kesi yake ya matunzo ya mtoto.

Hata hivyo, mamlaka ya polisi hata hivyo ilikanusha kuwa mwanablogu huyo alikuwa chini ya ulinzi wao.

Kulingana na Seneta wa Elgeiyo Marakwet Kipchumba Murkomen, Itumbi alipatikana amepigwa kikatili na kwa sasa anapokea matibabu hospitalini.

“Nimefurahi kumuona ndugu yetu Itumbi akiwa hai. Inasikitisha kumuona akiwa katika maumivu hayo. Natumai kwamba atarudi kwa nguvu zaidi. Alishtushwa na maafisa wa Polisi ambao wanapaswa kumlinda walimdhuru. Watesi wake wanaofurahia madaraka wasijue amani. Siasa hazifai kufanywa hivi,” Murkomen aliandika kwenye Twitter.