(Video) Mkutano wa Kalonzo wakatizwa na nyoka Kitui

Muhtasari

•Mkutano huo ulilazimika kusimama kwa muda kutokana na  hali ya mtafaruko iliyosababishwa na tukio hilo huku baadhi ya watu waliokuwa kwenye hema hilo wakijaribu kumuua nyoka huyo

Kiongozi wa Chama cha Wiper Kalonzo Musyoka akiwahutubia wakaazi wa Mukuru wakati wa ziara ya heshima ya kusambaza vyakula kwa waathiriwa wa ubomoaji katika eneo la Sisal eneo la Mukuru Kwa Njenga, Nairobi mnamo Januari 13, 2022.

Image: THE STAR

Kizaazaa kikubwa kilitokea katika mkutano wa kinara wa Wiper Kalonzo Musyoka ulioandaliwa nyumbani kwake Yatta baada ya nyoka kujitokeza kwenye hema walimokuwa wameketi viongozi.

Mkutano huo ulilazimika kusimama kwa muda kutokana na  hali ya mtafaruko iliyosababishwa na tukio hilo huku baadhi ya watu waliokuwa kwenye hema hilo wakijaribu kumuua nyoka huyo.

Katika video iliyoonekana na Radio Jambo, watu wachache waliokuwa wamehudhuria mkutano huo walionekana wakiwa wamejihami kwa miti wakikusudia kumuua mnyama huyo. Wengine walisikika wakipiga kelele 'SHINDWE! SHINDWE!'

Hatimaye mmoja wao alifanikiwa kumkamata nyoka huyo na kumpeleka mbali na mahali watu walikuwa wamekaa.