Msongamano mkubwa watarajiwa leo Mombasa Road huku ujenzi wa Expressway ukiingia awamu ya mwisho

Muhtasari

• Ujenzi wa barabara hiyo umesababisha mahangaiko miongoni mwa waitumiaji wake huku mkandarasi akiharakisha kumalizia kazi kabla ya kufunguliwa rasmi.

• Ujenzi wa barabara hiyo umesababisha mahangaiko miongoni mwa waitumiaji wake huku mkandarasi akiharakisha kumalizia kazi kabla ya kufunguliwa rasmi.

• Idara ya polisi imesema maafisa zaidi watatumwa huko kuelekeza madereva.

Image: CHARLEEN MALWA

Mamlaka ya Kitaifa ya Barabara Kuu nchini Kenya imetangaza kuwa itafunga sehemu ya Eastern Bypass Interchange leo Ijumaa usiku kuanzia saa nne hadi saa nane usiku (Januari 21) ili kufanikisha ujenzi wa kukamilisha Barabara ya Nairobi Expressway.

Kufunga kutafanyika katika eneo la City Cabanas. Huenda ikasababisha msongamano wa magari kwenye Barabara ya Mombasa ambayo tayari imekuwa ikishudia msongamano mkubwa hasa wakati huu wa mvua.

 Ujenzi wa barabara hiyo umesababisha mahangaiko miongoni mwa waitumiaji wake huku mkandarasi akiharakisha kumalizia kazi kabla ya kufunguliwa rasmi.

Idara ya polisi imesema maafisa zaidi watatumwa huko kuelekeza madereva.

Huku hayo yakijiri, barabara nyingi jijini Nairobi zimefurika maji kufuatia mvua iliyonyesha usiku wa kumkia Ijumaa.

Polisi wameonya kuwa hali hii itaathiri sana mtiririko wa trafiki na wanataka madereva kuchukua tahadhari.

 Iliyoathirika zaidi ni barabara ya Mombasa ambayo inaendelea kujengwa. Baadhi ya madereva walikaa barabarani kwa muda mrefu usiku wa kumkia Ijumaa kutokana na msongamano mkubwa wa magari katika sehemu kati ya Airtel na Mlolongo.

Kufuatia msongamano mkubwa wa magari katika barabara hiyo mamlaka ya viwanja vya ndege imewashauri wasafiri kufika JKIA saa tatu mapema kabla ya ,uda wa safari zao.