Jaguar ajiunga na Chama cha UDA

Muhtasari

•Habari za kuhama kwake  zilitangazwa kwenye ukurasa wa Twitter, Jumatatu asubuhi, na chama cha UDA .

•Hatua ya Jaguar inajiri siku chache baada ya mcheshi Jasper Muthomi, almaarufu Mc Jessy, kutangaza kuwa atawania kiti cha Imenti Kusini kwa tikiti ya chama cha UDA

Mheshimiwa Chalres Njagua akiwa na Naibu Rais Ruto
Mheshimiwa Chalres Njagua akiwa na Naibu Rais Ruto

Mbunge wa Starehe Chalres Njagua almaarufu Jaguar amejiunga rasmi na  chama cha Naibu Rais William Ruto, UDA.

Habari za kuhama kwake  zilitangazwa kwenye ukurasa wa Twitter, Jumatatu asubuhi, na chama hicho .

"The Hustler Nation inamkaribisha Mhe. Charles Kanyi Njagua Mbunge wa Starehe. Chama kinazidi kukua kwa kasi na mipaka huku viongozi wengi wakichagua kujiunga na kikosi cha washindi."

Hatua ya Jaguar inajiri siku chache baada ya mcheshi Jasper Muthomi, almaarufu Mc Jessy, kutangaza kuwa atawania kiti cha Imenti Kusini kwa tikiti ya chama cha UDA.

Mcheshi huyo alithibitisha Jumatano kwamba amejiunga rasmi na chama kinachongoozwa na  Ruto baada ya mashuriano mapana na wakazi wa eneo hilo.