Huduma ya Kitaifa ya polisi(NPS) imevunja kimya baada taarifa iliyotolewa na nchi za kigeni kwamba Raia wake ambao wanaishi humu nchini wajiepusha na baadhi ya sehemu humu nchini.
Msemaji wa Polisi Bruno Shioso ameeleza kuwa polisi wameimarisha ulinzi kote nchini na wamejipanga vyema kudhibiti shambulio lolote linalopangwa na wahauni.
"Idara yetu imehakikisha shughuli za usalama zinapewa kipaumbele, ambapo tutahakikisha kuwa hakuna mashambulizi yote yatazuiliwa," alisema Bruno Shioso.
Kauli hiyo inajiri saa chache baada ya Ufaransa kuwataka raia wake walio nchini Kenya kuwa waangalifu wanapozuru maeneo ya umma kwani kuna hatari ya kulenga maeneo ya umma yanayotembelewa na raia wa kigeni, haswa jijini Nairobi.
Katika taarifa iliyotolewa Alhamisi, Ufaransa ilisema kuwa mikahawa, hoteli, sehemu za burudani , vituo vya ununuzi ni miongoni mwa maeneo yaliyolengwa ambayo yanapaswa kuepukwa na raia wake.