Mfanyibiashara Chris Kirubi hakuacha mali yoyote kwa mkewe

Muhtasari

• Inaarifiwa kwamba marehemu mwanabiashara mkubwa nchini, Chris Kirubi hakuacha mali yoyote kwa mke wake na bibiye wa kando.

• Mwanabiashara huyo hakuwasahau ndugu na dada zake wanne huku kila mmoja akipata shilingi milioni mia tano, jambo ambalo wanawe wawili Robert na Mary-Anne walikubaliana nalo.

• Mwanabiashara huyu alikuwa na mashamba yenye dhamani ya shilingi bilioni 3.1 pamoja na lile la Loresho ambalo dhamani yake ni shilingi bilioni mbili huku lile la Kwale ambalo linakisiwa kuwa na dhamani ya shilingi milioni 11.

Inaarifiwa kwamba marehemu mwanabiashara ngili nchini, Chris Kirubi hakuacha mali yoyote kwa mke wake na bibiye wa kando.

Kirubi alifariki mwezi Juni mwaka jana akiwa ametimu miaka themanini, huku tangu siku hiyo wengi wakizidi kukuna vichwa kuhusu ni vipi mali zake zenye dhamani ya shilingi bilioni ishirini zingegawanywa miongoni mwa familia yake.

Kulingana na barua ya urithi aliyoiandika mwaka wa 1996, mfanyibiashara huyo aliwakabidhi mtoto wake wa kiume [Robert Kirubi] na bintiye [Mary-Anne] asilimia themanini ya nyumba zake huku akimpa msichana wake wa pili shilingi milioni nne.

Marehemu Kirubi hakuwasahau ndugu na dada zake wanne huku kila mmoja akipata shilingi milioni mia tano, jambo ambalo wanawe wawili Robert na Mary-Anne walikubaliana nalo.

“Tutashukuru iwapo utanakili mwafaka huu katika suala lililozungumziwa hapo juu. Kwamba agizo litolewe kuwa Fiona Wambui Kirubi atapokea asilimia 9.95 ya sehemu ya mali ya Robert Kirubi na Mary- Anne ikiwa ni asilimia themanini ya mali yote,” ridhaa hiyo ilisema.

Hiyo inamaanisha kwamba Fiona Kirubi atapokea shilling milioni 1.6 kutoka kwa ndugu zake.

Swali kuu linasalia kuwa mwanabiashara huyu mwenye upeo wa juu alimiliki nini haswa?

Kirubi, ambaye alikuwa mshika dau katika sekta mbalimbali za uwekezaji, zikiwemo uanahabari, uzalishaji wa bidhaa na teknolojia, alifanikiwa kuwa na hisa zenye dhamani ya shilingi bilioni 12.7.

Uwekezaji wake katika kampuni zilizoorodheshwa katika soko la hisa la Nairobi [NSE] ni wa thamani ya shilingi bilioni 3.4.

Alikuwa pia amewekeza zaidi ya shilingi milioni 1.8 katika kampuni ya kuzalisha dawa [Bayers East Africa Limited] ambayo iliasisi huduma zake humu nchini mnamo mwaka wa 1968.

KIRUBI
KIRUBI

Katika kampuni ya Haco, Kirubi alikuwa na hisa million 4.5 zilizokuwa na thamani ya shilingi milioni 801, huku kampuni za International House Limited na Kiruma International Limited zikikadiriwa kuwa na dhamani ya shillingi bilioni moja.

Pia alimiliki hisa 1,406 katika kampuni ya Bendor Estates Limited ambazo dhamani yake ni shilingi bilioni 5.6.

Mfanyibiashara huyo alikuwa na mashamba yenye thamani ya shilingi bilioni 3.1 pamoja na lile la Loresho ambalo thamani yake ni shilingi bilioni mbili huku lile la Kwale ambalo linakisiwa kuwa na thamani ya shilingi milioni 11.

Mali zingine katika mtaa wa kifahari wa Muthaiga na Mtwapa zina dhamani ya shilingi milioni 60 kila moja.

Ikumbukwe kwamba pia alimiliki magari sita yenye ghali yakiwemo: Mercedes Benz Maybach S500 [shilingi milioni 30], He also owned 6 six high-end cars: Mercedes Benz Maybach S500 (Sh30 million), Bentley Continental GT (shilingi milioni 29), Range Rover (shilingi milioni 26), Mercedes Benz (shilingi milioni 16), Mercedes Benz ML 320 CDI (shilingi milioni tano) na Mercedes CLS 350 [shilingi milioni tatu].