Lori la mafuta lagonga duka la majeneza na kuua mwanamke mmoja, Nyamira

Muhtasari

•Lori hilo ilikuwa likielekea mjini Nyamira wakati dereva alipoteza mwelekeo na kugonga duka la kuuza majeneza.

•Mtoto wa marehemu, nyanyake, dereva na kondakta wake wanapokea matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Kaunti ya Nyamira.

Meli ya mafuta ambayo iligonga duka la majeneza na kumuua mtu mmoja huko Nyamira mnamo Machi 30, 2022.
Meli ya mafuta ambayo iligonga duka la majeneza na kumuua mtu mmoja huko Nyamira mnamo Machi 30, 2022.
Image: ALVIN RATEMO

Mtu mmoja alifariki na wengine wanne kujeruhiwa baada ya lori la mafuta kugonga nyumba katika mji wa Kebirigho, kaunti ya Nyamira.

Lori hilo ilikuwa likielekea mjini Nyamira wakati dereva alipoteza mwelekeo na kugonga duka la kuuza majeneza.

Maduka kadhaa na nyumba zingine pia ziliharibiwa katika tukio hilo la Jumatano asubuhi. Mwanamke ambaye aliuza duka lililo karibu na duka hilo la majeneza alifariki huku mtoto wa miaka minne akiuguamajeraha.

Kamanda wa Polisi wa Kaunti Ndogo ya Nyamira Kaskazini, Patrick Ngeiywa alisema kuwa mwanamke huyo alikuwa ndani ya duka lake.

Kulingana na Ngeiywa, lori hilo ilikuwa likielekea Kisii kutoka Nakuru wakati a ajali hiyo kutokea. Mtoto wa marehemu, nyanyake, dereva na kondakta wake wanapokea matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Kaunti ya Nyamira.

Maafisa wa polisi walifika eneo la tukio kwa wakati ili kudhibiti umati wa watu waliokuwa wamekusanyika kuchota mafuta kutoka kwa lori hilo.