Bei ya mafuta bado haijabadilika licha ya Serikali kutoa mapungufu ya Sh16b

Wakenya washangaa kuhusu ahadi ya Serikali kuhusu mafuta

Muhtasari

•Mwezi uliopita, EPRA ilitangaza kupanda kwa bei ya mafuta kwa Sh9 kwa lita.

•Ahadi ya Serikali kuhusu  bei ya Mafuta nchini.

 

Mhudumu katika kituo cha Mafuta
Mhudumu katika kituo cha Mafuta
Image: STAR

Bei za mafuta zitasalia bila kubadilika hadi Agosti 14, Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Petroli (EPRA) ilitangaza Alhamisi.

EPRA ilisema serikali imetoa Sh16.675 bilioni ili kuwaepusha Wakenya kutokana na bei ya juu ya mafuta.

Petroli sasa itauzwa kwa Sh159.12, Mafuta ya Taa Sh127.9 4 na dizeli kwa Sh140.00.

Bila mapungufu  bei ingeongezeka hadi Sh193.64 kwa dizeli, sh209.95 kwa petroli na Sh 181.13 kwa Mafuta ya Taa.

Mwezi uliopita, EPRA ilitangaza kupanda kwa bei ya mafuta kwa Sh9 kwa lita.

Mabadiliko ya bei yalitazamiwa kuanzia Juni 15 hadi Julai 14, 2022.

Mamlaka hiyo  ilisema kuwa serikali itatumia Tozo ya Maendeleo ya Petroli (PDL) ili kuwaepusha wateja na bei hizo za juu.