Mtu mmoja amefariki, huku wanafunzi wakipata majeraha katika ajali

waliopata majeraha walikimbizwa katika hospitali ya kaunti ya Murang'a.

Muhtasari

•Magari ya uchukuzi hayo mawili yalikuwa matatu  kutoka 2NK Sacco, ambayo yalikuwa yakiwasafirisha wanafunzi tofauti kuwapeleka shuleni.

Ajali barabarani
Ajali barabarani
Image: HANDOUT

Huzuni ilitanda eneo la Sagana kaunti ya Murang'a baada ya mtu mmoja kufariki kufuatia ajali iliyotokea Alhamisi alasiri, Agosti 18.

Ajali hiyo lilitokea wakati lori lilipogongana na Magari mawili ya Watumishi wa Umma (PSV) na magari manne ya kibinafsi huko Kambiti, kando ya barabara kuu ya Nairobi-Meru.

Ripoti za vyombo vya habari zilisema kuwa lori hilo lililokuwa likisafirisha bia, lililokuwa likielekea Sagana, lilipoteza mwelekeo baada ya breki kufeli, na kuyagonga magari mengine sita.

Magari ya uchukuzi hayo mawili yalikuwa matatu  kutoka 2NK Sacco, ambayo yalikuwa yakiwasafirisha wanafunzi tofauti kuwapeleka shuleni.

Miongoji mwa waathiriwa wa ajali hiyo walikuwa wanafunzi kutoka shule za upili ya Nyeri , Endarasha, na Kaheti.

Kulingana na maafisa wa polisi waliozungumza na wanahabari, waliopata majeraha walikimbizwa katika hospitali ya kaunti ya Murang'a.

Haya yanajiri baada ya waziri wa elimu profesa George Magoha kutoa taarifa kwa umma kuwataka wanafunzi kurejelea masomo kwanziac Alhamisi Agosti 18 baada ya kukaa nje kwa takribani majuma mawili ili kupisha tume huru ya mipaka na uchaguzi IEBC kutumia baadhi ya shule hizo kama vituo vya kupigia kura.

Awali, Magoha alikuwa amekanganya wazazi na washikadau katika sekta ya elimu kwa kubadilisha tarehe mwanzo kutoka Agosti 11 hadi Agosti 15 kabla ya kubadilisha tena na kusema Agosti 18.

Katika sehemu nyingi za nchi Alhamis asubuhi iliona wanafunzi wengi wakifurika vituo vya kuabiri magari ili kutii agizo la waziri Magoha kuwataka warudi shuleni kuendelea na sehemu ya muhula huu iliyosalia.