Mwanamume ajitia kitanzi baada ya jaribio la kuua wanawe 4 kutibuka, Homabay

Baba alikunywa sumu kabla ya kujaribu kuwaua watoto wao wanne.

Muhtasari

• Watoto hao wanazidi kupata matibabu kwenye hospitari rufaa ya Homabay.

• Mzee huyo alikuwa anafaa kufika kwenye idara ya watoto kujibu madai ya mzozo wa kinyumbani.

Image: DCI

Wakaazi wa kijiji cha Rangwe kaunti ya Homabay wamepigwa na butwaa baada ya mwanamume mwenye umri wa miaka 40 kujaribu kuwaua wanawe kabla ya kujitoa uhai. 

Ronny Ochieng, aliwadunga kisu tumboni wanawe wawili ambao ni mapacha  wa kiume wa miaka 3 kabla ya kuwapa sumu binti zake wawili wenye umri wa miaka 5 na 9.

Kulingana na ripoti iliyotolewa na maafisa wa upelelezi, baba huyo alikunywa sumu.

Majirani waliosikia vilio vya watoto hao na kuwakimbiza katika hospitalini ya Homabay ambapo wanapokea matibabu huku wakiwa katika hali mbaya.

Ripoti ya DCI ilisema baba huyo katili alitangazwa kufariki alipofika katika hospitali ya Homabay. Mama yao hakuwepo wakati wa tukio hilo. 

Maafisa wa upelelezi waliongeza kuwa mzee huyo alikuwa ameagizwa kufika katika Afisi ya Idara ya Watoto mjini Rangwe Desemba 14 kwa madai ya kutekeleza dhulma za kinyumbani.