Ruto avunja kimya kuhusu kuteswa kwa mtoto Junior Sagini

Rais aliwasihi Wakenya kuwatunza watoto wote.

Muhtasari

•Rais William Ruto aliwashutumu wazazi na walezi wa mtoto huyo wa miaka mitatu kwa kushindwa kumlinda.

•Aliuliza ni shetani  mgani anayemwingia mwanadamu hadi kumfanya ammdhuru mtoto mdogo asiye na hatia.

RAIS WILLIAM RUTO
Image: TWITTER

Rais William Ruto amechangia katika kesi ya mateso kwa Mtoto Juniour Sagini ambayo yalimuacha kipofu baada ya macho yake kung'olewa.

Rais aliwashutumu wazazi na walezi wa mtoto huyo wa miaka mitatu kwa kushindwa kumlinda.

Wakati akizungumza katika makao ya watoto ambayo alitembela mjini Eldoret siku Ijumaa, Ruto aliwasihi Wakenya kuwatunza watoto wote.

"Tafadhali watunzeni Watoto wetu," alisema.

Alisema anashangaa wapo wazazi wanaohatarisha maisha ya watoto wao badala ya kuwalinda.

“Tumeona kuna mzazi mmoja huko Kisii ambaye amemtoa macho mtoto wao. Ni jambo la kushangaza sana kufanya,” alisema.

Aliuliza ni shetani wa aina gani anayemwingia mwanadamu hadi kumfanya ammdhuru mtoto mdogo asiye na hatia na kuharibu maisha yao.

"Na wazazi wengine wanapowaumiza watoto wao, tuna watu wema kama hawa (nyumba ya watoto) ambao wanachukua watoto bila wazazi na kuwalea. Kwa kweli ni ulimwengu wa tofauti,” alisema.

Ruto alisema kuwa atahakikisha kuwa Serikali inatekeleza Mswada wa Watoto uliopitishwa hivi majuzi ambao unalinda haki za watoto.

“Serikali itaweka mipango ya kuhakikisha kuwa hakuna mtoto nchini Kenya anayelelewa vibaya au kuumizwa au kudhulumiwa ama na wazazi au na mtu yeyote. Serikali ya Kenya italinda watoto wake,” alisema.

Utafsiri: Samuel Maina