Berlin Marathon: Mamilioni Eliud Kipchoge ataweka mfukoni kama pesa za zawadi

Kwa wanaume na wanawake walioshinda mbio hizo, ripoti nyingi zinaonyesha kuwa kila mmoja atapata zawadi ya $50,000 (Sh7.3 milioni).

Muhtasari

• Wanariadha waliomaliza wa pili watajipatia dola 25,500 (Sh milioni 3.7) huku watakaoshika nafasi ya tatu watapata dola 12,500 (Sh milioni 1.8).

Elidu Kipchoge.
Elidu Kipchoge.
Image: Hisani

Kenya ilichomoza tena katika kilele cha kimataifa siku ya Jumapili baada ya Eliud Kipchoge kushinda mbio za rekodi ya tano za Berlin Marathon.

Bingwa wa mara ya tano wa Berlin Marathon bila shaka ataondoka nyumbani na kiasi kizuri cha pesa.

Ingawa kiasi cha mfuko mmoja kinatofautiana, The Star waliweza kubaini pesa ambazo wanariadha bora wataweka mfukoni kwa mafanikio yao katika mbio hizo.

Kwa wanaume na wanawake walioshinda mbio hizo, ripoti nyingi zinaonyesha kuwa kila mmoja atapata zawadi ya $50,000 (Sh7.3 milioni).

Kiasi hicho kinatarajiwa kuwa zaidi kwa atakayevunja rekodi ya dunia.

Hii inamaanisha kuwa Kipchoge atapata Sh7.3 milioni. Kwa jumla, atapata zaidi kutokana na mikataba ya udhamini na gharama za ushiriki.

Wanariadha waliomaliza wa pili watajipatia dola 25,500 (Sh milioni 3.7) huku watakaoshika nafasi ya tatu watapata dola 12,500 (Sh milioni 1.8).

Wanariadha walioshika nafasi ya nne, kila mmoja atajinyakulia dola 7,500 (Sh milioni 1.1) huku wale wa tano wakiwa na dola 5,000 (Sh 726,000).

Kutoka nafasi ya sita hadi ya 10, wanariadha watatia mfukoni $3,000 (Sh 435,630).

Mwanariadha bora zaidi duniani Eliud Kiopchoge ameendeleza wimbi lake la ushindi baada ya kushinda mbio za Berlin Marathon.

Alitumia saa 2:02:42.

Mkenya mwingine Vincent Kipkemboi aliibuka wa pili baada ya kutumia saa 2:03:13.

Hii hapa ni orodha ya waliomaliza 10 bora:

1. Eliud Kipchoge Kenya 2:02:42

2. Vincent Kipkemoi Kenya)2:03:13

3. Tadese Takele  Ethiopia 2:03:24

4. Ronald Korir Kenya 2:04:22

5. Haftu Teklu Ethiopia 2:04:42

6. Andualem Shiferaw Ethiopia 2:04:44

7. Amos Kipruto Kenya 2:04:49

8. Philemon Kiplimo Kenya 2:04:56

9. Amanal Petros  Germany 2:04:58

10. Boniface Kiplimo Kenya 2:05:05