LIGI KUU UINGEREZA

Young asajiliwa tena kwenye ligi kuu nchini Uingereza

Mchezaji huyo ametia saini mkataba wa mwaka mmoja na klabu ya Aston Villa

Muhtasari

•Aliyekuwa mlinzi wa Manchester United, Ashley Young amerudi tena kwenye ligi kuu ya Uingereza baada kuchezea Inter Milan ya Italia kwa misimu miwili.

•Young anajiunga na Villa siku chache tu baada ya klabu hiyo kusahili kiungo matata wa Norwich City, Emiliano Buendia.

Ashley Young
Ashley Young
Image: Twitter

Aliyekuwa mlinzi wa Manchester United, Ashley Young amerudi tena kwenye ligi kuu ya Uingereza baada kuchezea Inter Milan ya Italia kwa misimu miwili.

Young ambaye ana umri wa miaka 35 amesajili na klabu ya Aston Villa ambayo aliwahi kuichezea kwa kipindi cha miaka mitano(2007-2011) kabla ya kujiunga na Manchester United.

Mchezaji huyo raia waUingereza ametia saini mkataba wa mwaka mmoja na klabu hiyo inayoongozwa na kocha Dean Smith.

"Ashley analeta umaarufu mkubwa kwenye klabu hii na anajiunga nasi baada ya kushinda ligi nchini Italia. Ni mchezaji ambaye anaweza cheza katika safu mbalimbali. Baada ya kushiriki mazungumzo naye najua ataleta matokeo mazuri msimu huu" Kocha Dean Smith alisema wakati mchezaji huyo alizinduliwa kwenye klabu ya Aston Villa.

Young anajiunga na Villa siku chache tu baada ya klabu hiyo kusahili kiungo matata wa Norwich City, Emiliano Buendia.

Klabu hiyo imeonekana kuendelea kuimarisha kikosi chake na huenda ikawa tishio kwa vilabu vingine nchini Uingereza  kwenye msimu unaoanza tarehe 14 mwezi Agosti.