Otamendi usimjeruhi Messi maana nitakuua, Kombe la Dunia linakuja - Aguero

Messi wa PSG watakutana na Otamendi wa Benfica katika kipute cha Champions League wiki chache kabla ya ujio wa kombe la dunia

Muhtasari

• Aguero alimuonya Otamendi wa Benfica dhidi ya kumjeruhi Messi wa PSG timu hizo zitakapokutana katika mechi ya klabu bingwa Uropa.

• Wachezaji hao wote ni wa timu ya taifa ya Argentina na Aguero alimuambia achunge kutomjeruhi kwani kipute cha kombe la dunia kinakuja Novemba.

Aguero alimuonya Otamendi dhidi ya kumjeruhi Messi wakati wa Champions League
Messi, Aguero Aguero alimuonya Otamendi dhidi ya kumjeruhi Messi wakati wa Champions League
Image: Gatty Images//BBC

Usiku wa kuamkia leo, droo ya kipute cha kombe lenye maskio marefu zaidi barani Uropa kwa maana ya Klabu bingwa ilifanyika mjini Istanbul ambapo sasa ni rasmi kila timu ambayo ilimaliza miongoni mwa nne bora katika ligi kuu za mataifa ya Uropa zimejua wapinzani wao.

Katika kundi H ambalo liliwakutanisha miamba wa Italia Juventus, vigogo wa Ufaransa PSG, Benfica ya Ureno na Maccabi Haifa ya Israeli ni kundi ambalo limemuacha mchezaji wa zamani wa Manchester City na Barcelona, Kun Aguero akizungumza kwa onyo kali kwa baadhi ya wachezaji.

Kundi hilo linawakutanisha wachezaji wa timu ya taifa ya Argentina ambao ni nguli wa shughuli hizo Lionel Messi wa PSG, Angel Di Maria wa Juventus na Nicholas Otamendi anayekipiga kule Benfica.

Licha ya kuwa wachezaji kutoka taifa moja wanaowakilisha timu ya taifa, lakini katika kipute hiki watakuwa wanacheza kama maadui kila mmoja akijaribu kusaidia klabu yake kufuzu Kwenda kiwango kingine.

Hili limemfanya Aguero kutoa onyo kali haswa kwa Otamendi na kumuambia asidhubutu kumtia jeraha nahodha wa timu ya taifa Lionel Messi Benfica watakapokutana na PSG kwani mwezi Novemba mashindano ya kombe la dunia yatafanyika Qatar.

Katika video ambayo imepakiwa sana kweney mitandao ya Twitter na Instagram, Agueor anamuona vikali Otamendi dhidi ya kufanya udhubutu wa kumjeruhi Messi na kumtania kwamba atamuua endapo atafanya hivyo.

“Otamendi usimjeruhi Leonel Messi maana nitakuua. Kombe la Dunia linakuja,” Aguero anaonekana kwenye video akisema kwa lugha ya Kiargentina ambayo baadae ilitafsiriwa kwa Kiingereza.