(video) Shabiki aingia uwanjani, achomoa kibendera cha kona na kumpiga golikipa vibaya

Shabiki huyo alionekana kukimbia kutoka pembezoni mwa uwanja kabla ya kuchukua mlingoti wa kibendera cha kona na kumtwanga vikali golikipa.

Muhtasari

• Shabiki huyo aliangusha vipigo viwili vizito mgongoni mwa Ozan, golikipa, kabla ya kuzuiwa na usalama na wachezaji wengine.

Huku ligi kuu kote duniani zikiwa zimesitishwa kupisha mashindano ya kombe la dunia, nchini Uturuki, ligi bado inaendelea.

Katika mechi iliyozikutanisah timu za Gotzepe na Altay Jumapili, mechi hiyo ilikumbwa na visa kadhaa vya vurugu na fujo uwanjani mpaka kupelekea kusitishwa kwake.

Video moja ambapo imesambazwa mitandaoni na ambayo inakisiwa kuchukuliwa kutoka kwa moja ya matukio ya vurugu katika uwanja huo, golikipa alionekana akishambuliwa vikali na mtu aliyechukua beramu ya pembezoni mwa uwanja kabla ya kumtwanga nayo kichwani kwa nguvu zote.

Goztepe walikuwa wakiwakaribisha Altay kwenye Uwanja wa Gürsel Aksel Stadyumu na hakuna mtu ambaye angeweza kufikiria kuwa tukio hilo la kushtua lingeweza kutikisa mchezo. Kweli, isipokuwa labda kwa shabiki.

Sports Brief Kenya waliripoti kwamba mchezo huo ulikumbwa na shabiki aliyedhaniwa kuwa wa Altay alirusha moto uliomshika shabiki wa timu nyingine usoni. Mchezo huo ulisimamishwa kwa muda huku msaada wa kimatibabu ulikitafutwa kwa mashabiki walioathirika.

Katika tukio hilo, ambulensi iliingia uwanjani huku wachezaji na mashabiki wakizingira kabla ya jamaa mmoja kuonekana kukimbia kutoka pembezoni mwa uwanja na kibendera cha kona ambacho alitumia mlingoti wake kumpiga vikali golikipa wa timu pinzani.

Shabiki huyo aling'oa bendera ya kona alipokuwa akienda na kumshambulia vibaya Ozan, golikipa wa Altay kwa nyuma. Shabiki huyo aliangusha vipigo viwili vizito mgongoni mwa Ozan kabla ya kuzuiwa na usalama na wachezaji wengine.