Hakuna kushiriki mazoezi: Baadhi ya 'ushirikina' wa Mourinho kuelekea Fainali

Huku Roma wakijiandaa kushuka dimbani dhidi ya Sevila kwenye fainali, Mourinho ametoa amari kama ya mwaka jana kwenye fainali ya Conference kupiga marufuku mazoezi.

Muhtasari

• AS Roma ya Mourinho inajiandaa kushuka dimbani usiku wa Jumatano kumenyana na Sevilla kwenye fainali ya kombe la Uropa.

• José Mourinho hajawahi kupoteza fainali ya Uropa na kwa upande mwingine Sevilla imeshinda mechi zote sita za fainali za Ligi ya Europa.

Mourinho ailinganisha kazi yake Roma kama Yesu kutembea Vatican
Mourinho ailinganisha kazi yake Roma kama Yesu kutembea Vatican
Image: Twitter

Huku AS Roma kutoka Italia wakijiandaa kushuka dimbani dhidi ya Sevilla ya Uhispania kweney fainali ya kombe la Uropa, inaripotiwa kwamab kocha mkuu wa Roma, Jose Mourinho amepiga baadhi ya watu marufuku kwenye timu hiyo dhidi ya kushiriki katika mazoezi.

Hili linatajwa kuwa moja ya ‘ushirikina’ wa Mourinho kila wakati timu anayoingoza inapojiandaa kushiriki katika fainali ya kombe muhimu barani Ulaya.

Kulingana na jarida la Mirror la Uingereza, Mourinho ametangaza marufuku kwa baadhi ya wafanyikazi wa timu ya Roma kuingia kwenye uwanja wa mazoezi huko Budapest ambapo fainali inatarajiwa kuchezwa usiku wa Jumatano.

Bosi huyo wa Ureno amechukua hatua kali ili kuhakikisha mafanikio, huku Corriere Dello Sport ikiripoti kuwa sera hiyo iliwekwa Jumatatu.

Wafanyikazi muhimu pekee ndio wanaoaminika kuwa wameruhusiwa katika kituo chao cha mafunzo kwa vikao wiki hii, na wafanyikazi wa kiufundi na wa matibabu pekee wanaruhusiwa kuingia.

Inaripotiwa kuwa pia Mourinho aliweka amri kama hii mwaka jana wakati wa kuiongoza Roma kutwaa ubingwa wa Europa Conference dhidi ya Feyenoord.

“Huu ndio ukubwa wa mechi ya Budapest Jumatano, hatua hiyo ni ishara ya ushirikina wa Mourinho katika maandalizi ya fainali. Alichukua hatua kama hizo mwaka jana katika maandalizi ya fainali ya Ligi ya Europa, ambayo Roma ilishinda dhidi ya Feyenoord na kufanikiwa kutwaa taji lao la kwanza tangu 2008,” jarida hilo liliripoti.

Mourinho mara nyingi amekuwa akistawi wakati mabeki wako kwenye ukuta, na mbinu hii inakumbusha mawazo ya kuzingirwa ambayo mara nyingi yamekuwa yakitoa matokeo kwa meneja huyo mwenye haiba.

José Mourinho hajawahi kupoteza fainali ya Uropa na kwa upande mwingine Sevilla imeshinda mechi zote sita za fainali za Ligi ya Europa.