SOKA KIMATAIFA

Laana ya Mwafrika kwa Pep ilifutwa au bado ipo?

Hutawahi shinda taji la Champions League

Muhtasari

•Inaaminika kuwa, Guardiola amejaribu kulinyakua taji hilo akiwa City misimu yote ambayo amekuwa humo bila kufanikiwa kutokana na laana ya Mwafrika Yaya Toure.

•Amedhalilisha bara zima la Afrika” Alisema Dimitiri Seluk ajenti wa Toure wakati huo.“ Kwa hiyo Waafrika hataruhusu Guardiola kulibeba taji la Champions League.”

katika siku zake Man City.
Pep Guardiola na Yaya Toure katika siku zake Man City.
Image: HISANI

Huku zikiwa zimesalia siku mbili ndipo kuandaliwa kwa fainali ya kombe la EUFA mjini Istanbul, maswali yanaoibuka na kumtia wasiwasi meneja wa Man City Pep Guardiola ni kuwepo kwa usemi wa laana dhidi yake.

Inaaminika kuwa, Guardiola amejaribu kulinyakua taji hilo akiwa City misimu yote ambayo amekuwa humo bila kufanikiwa kutokana na laana ya Mwafrika Yaya Toure.

Toure, mwenye uraia wa Ivory Coast alikuwa mmoja wa wachezaji waliosifiwa sana na klabu ya Man City. Nyota huyo, aliisaidia City katika msimu wa 2013/2014  ligi kuu Uingereza kunyakua taji, wakati ambapo alifunga mabao 20 akawa miongoni mwa wafungaji bora kwenye ligi.

Kujili kwa Mhispaniola huyo kwenye City, alianzisha madiliko ambapo wachezaji wengi walisajiliwa huku wengine wakifurushwa. Ingawa Toure alicheza misimu miwili chini ya ukufunzi wa Pep, mambo hayakuwa kama yalivyokuwa chini ya meneja Manuel Pellegrini, maana msimu wa 2017/2018 kiungo huyo alianza mara moja tu msimu mzima.

Tukio hili lilimghadhabisha sana Toure hadi alipoondoka ugani Etihad na ambapo aliyekuwa ajenti wake wakati huo akisema kuwa Guardiola amelidhalilisha bara la Afrika.“ Amedhalilisha bara zima la Afrika” Alisema Dimitiri Seluk ajenti wa Toure wakati huo.“ Kwa hiyo Waafrika hataruhusu Guardiola kulibeba taji la Champions League” Aliendelea.

Ingawa nyota huyo wa zamani wa Man City kupitia mtandao wa Twitter alisema kwamba hana kinyongo na meneja huyo, iwapo ameitupilia lawama hiyo kutabainika Juni 10 katika fainali ya EUFA dhidi ya Inter Milan.

Toure alisema kwamba hana ubaya wa Man City na pia anatumai watashinda taji hilo msimu huu.