Ronaldo aliangushwa na kupewa penalti lakini akamwambia refa penalti hiyo si halali

Mchezaji huyo alikuwa ameangushwa ndani ya boksi na refa akamzawadi penalti lakini akaungana na wachezaji wa timu pinzani kuikataa penalti hiyo kuwa ni haramu hivyo kupelekea refa kuibatilisha.

Muhtasari

• Beki wa Al Nassr alikuwa amelambishwa kadi nyekundu na hivyo Ronaldo na wenzake kusalia 10 uwanjani na mpaka anaangushwa ndani ya kijisanduku, walikuwa sare kapa.

Christiano Ronaldo
Christiano Ronaldo
Image: Facebook

Kwa mara nyingine tena staa wa kabumbu wa muda wote kutokea Ureno, Christiano Ronaldo ameonesha sababu ya kuheshimiwa katika malimwengu ya soka kwa kumwambai refa kuwa penalti aliyomzawidi si halali.

Mchezaji huyo alizua kioja uwanjani usiku wa Jumatatu katika mechi za ligi ya mabingwa barani Asia, AFC nchini Iran wakati wa mechi ya timu ya Persepolis dhidi ya Al Nassr ya Ronaldo.

Beki wa Al Nassr alikuwa amelambishwa kadi nyekundu na hivyo Ronaldo na wenzake kusalia 10 uwanjani na mpaka anaangushwa ndani ya kijisanduku, walikuwa sare kapa.

Ghafla refa akapuliza kipenga na kusema kwamba mchezaji huyo alichezewa madhambi ndani ya boksi na kuwapa Al Nassr penalty, lakini Ronaldo akainuka na kuelekea kwa refa akimwambia kwamba hiyo haikuwa penalty halali na hivyo kumsaidia refa katika kurudisha maamuzi yake.

Mwamuzi Ma Ning aliangalia mfuatiliaji wa uwanja na kubatilisha uamuzi wake.

Beki wa Al-Nassr Ali Lajimi alitolewa kwa kadi nyekundu katika kipindi cha pili kwa kumchezea vibaya Milad Sarlak, na Ronaldo aliitoa timu yake ya Saudi Arabia hofu alipotoka kwa jeraha la shingo.

Lakini Al-Nassr walikuwa tayari wamefuzu kwa hatua ya mtoano kama mshindi wa Kundi E na kusonga mbele bila kushindwa.

Timu ya Riyadh iliingia kwenye mchezo huo ikiwa imeshinda michezo 18 kati ya 19 ya awali katika mashindano yote.

Katika kundi hilo hilo, Al-Duhail ya Qatar ilipata ushindi wake wa kwanza baada ya kuishinda Istiklol ya Tajikistan mabao 2-0. Mshambulizi mahiri Mkenya Michael Olunga alifunga mabao yote mawili.