Ronaldo atumia mtindo mchafu kusherehekea na kuwazima mashabiki wa Messi

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 39 alionekana akinyoosha mkono wake kuelekea kwa wafuasi wa Al Shadab kabla ya kurudia kusukuma mkono wake mbele ya eneo la fupanyonga.

Muhtasari

• Kwa muda wote, mashabiki walisikika wakipiga kelele 'Messi' - mpinzani wa muda mrefu wa Ballon d'Or wa Ronaldo wakati alipokuwa kwenye soka la Ulaya.

Ronaldo
Ronaldo
Image: X

Cristiano Ronaldo anatarajiwa kuchunguzwa baada ya kuonekana akitoa ishara chafu kujibu mashabiki kwenye mchezo wa Saudi Pro League waliokuwa wakiimba nyimbo za kumsifu Messi – mpinzani wake wa muda wote.

Gazeti la Saudi Arabia, Asharq al-Awsat  linabainisha kuwa Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ureno alianza kuifungia Al Nassr katika ushindi wa 3-2 dhidi ya Al Shadab Jumapili, kwa bao la pili lililofungwa na Anderson Talisca kipindi cha pili na kupata pointi zote tatu.

Kwa muda wote, mashabiki walisikika wakipiga kelele 'Messi' - mpinzani wa muda mrefu wa Ballon d'Or wa Ronaldo wakati alipokuwa kwenye soka la Ulaya - na video kwenye mitandao ya kijamii zilinasa hisia za fowadi huyo wa zamani wa Real Madrid, Manchester United na Juventus.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 39 alionekana akinyoosha mkono wake kuelekea kwa wafuasi wa Al Shadab kabla ya kurudia kusukuma mkono wake mbele ya eneo la fupanyonga.

Gazeti la Saudi Asharq al-Awsat linadai shirikisho la soka la nchi hiyo (SAFF) limefungua uchunguzi, huku baadhi ya wadadisi kutoka eneo hilo wakiamini Ronaldo anapaswa kupata adhabu licha ya hadhi yake ya juu miongoni mwa wachezaji waliosajiliwa na Saudia Pro League katika miaka ya hivi karibuni.

Sio mara ya kwanza kwa Ronaldo kujitumbukiza kwenye maji moto.

Alionekana kushika sehemu zake za siri akielekea nje ya uwanja mwishoni mwa kichapo cha 2-0 kutoka kwa Al Hilal mwezi Aprili, huku akiishusha skafu ya timu hiyo kwenye kaptura yake kisha kuitupa baada ya Al Nassr kupoteza 2- 0 katika fainali ya Kombe la Msimu wa Riyadh.

Huku Ronaldo akiwa ndiye kinara wa mabao kwa sasa kwenye Ligi ya Saudia msimu huu akiwa amefunga mabao 22, timu yake ya Al Nassr ipo nyuma kwa pointi saba dhidi ya Al Hilal kileleni mwa jedwali.

Mshindi huyo mara nne wa tuzo ya Ballon d'Or atakuwa akitazama mabao mengine au mawili siku ya Alhamisi wakati timu yake itakapomenyana na Al Hazem, ambayo inashika nafasi ya mwisho kwenye msimamo wa ligi kuu ya Saudi Arabia ikiwa na pointi 14 pekee kati ya michezo 21.