ODM yakana kutoa orodha ya wagombeaji waliopewa tikiti ya moja kwa moja

Muhtasari

• Mkurugenzi wa mawasiliano wa ODM Phillip Etale siku ya Jumanne aliambia meza ya habari ya Radio Jambo kwamba orodha hiyo ni bandia na haijatolewa na chama ODM.

• Kulingana na Etale ODM haijampa mtu yeyote tiketi ya moja kwa moja kwa uchaguzi wa Agost 9, mwaka huu.

Image: ODM/TWITTER

Chama cha ODM kimejitenga na orodha ya wagombeaji ambayo imekuwa ikisambazwa  mitandaoni ikidai kuwa baadhi ya wagombeaji wamepewa uteuzi wa moja kwa moja bila kupitia mchujo.

Mkurugenzi wa mawasiliano wa ODM Phillip Etale siku ya Jumanne aliambia meza ya habari ya Radio Jambo kwamba orodha hiyo ni bandia na haijatolewa na chama ODM.

Kulingana na Etale ODM haijampa mtu yeyote tiketi ya moja kwa moja kwa uchaguzi wa Agost 9, mwaka huu.

Orodha hiyo ambayo imekuwa ikisambazwa katika mitandao inayonyesha kuwa baadhi ya wagombeaji  miongoni mwao gavana wa Kajiado Joseph Ole Lenku, Mbunge wa Embakasi East Babu Owino, Simba Arati wamepewa tiketi za moja kwa moja.

Ujumbe katika orodha hiyo ulidai kwamba chama cha ODM kitawarejeshea ada za uteuzi wagombeaji wengine ambao walikuwa wamewailisha maombi ya kuania nyadhifa ambazo zimeathirika na uteuzi ya moja moja.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Madai haya yalijiri muda mchache tu baada ya aliyekuwa msemaji wa idara ya polisi Charles Owino kujiondoa kutoka uteuzi wa chama cha ODM.

Owino siku ya Jumanne alijiondoa kutoka kinyang’anyiro cha kuania ugavana wa kaunti ya Siaya na kuungana na mgombea wa kiti hicho kwa tiketi ya chama cha UDM Nicholas Gumbo.

Gumbo awali alikuwa amehusishwa na chama cha mbunge wa Ugenya David Ochieng MDG naye Owino alikuwa tayari amelipa ada za uteuzi kwa chama cha ODM.

Wawili hao walilakiwa katika chama cha UDM na gavana wa Mandera Ali Roba katika makao makuu ya chama hicho mjini Nairobi.

"Sababu kuu iliyotufanya tujumuike pamoja ni kwamba tumeona kutakuwa na ususiaji wa kupiga kura miongoni mwa wafausi wetu, wafuasi wetu wamekuwa wakilalamika kuwa hawatapiga kura bila sisi kupiga kura," Owino alisema.