UDA: Wagombea walioshiriki kuteketeza Karatasi za kupiga kura za mchujo kufunguliwa mashtaka

Image: BENJAMIN MUNENE

Muungano wa United Democratic Alliance (UDA) umetoa wito kwa wanachama wake watatu kuhusu machafuko yaliyotokea nje ya Izaak Walton Inn katika mji wa Embu.

Margaret Lorna Kariuki (Mbunge Mteule wa Bunge la Kaunti), John Muchiri Nyaga (Mbunge wa Manyatta) na Norman Nyaga (mwanasiasa wa UDA) waliagizwa Jumatano kufika mbele ya kamati ya nidhamu ya chama hicho kwa madai ya uchomaji wa kimakusudi na uharibifu wa Karatasi za kupiga kura za mchujo.

Taarifa iliyotolewa inasema kwamba kuna ushahidi wa kanda za video, habari na nyenzo zinazowahusisha watatu hao na tukio hilo.

“Kamati ya nidhamu inakuiteni kufika mbele yake Jumamosi, Aprili 16 saa 9:00 asubuhi kwa ajili ya kusikizwa kwa kesi hiyo katika Kituo cha Hustlers kwenye Barabara ya Makindi karibu na Barabara ya Riara jijini Nairobi,” taarifa hiyo ilisema.

Watatu hao walionywa kuwa iwapo madai hayo yatathibitishwa, wataondolewa kwenye uteuzi huo na watakabiliwa na ama kusimamishwa au kufukuzwa katika chama.

Kariuki, Muchiri na Nyaga wanaweza kufika kibinafsi au kuleta pamoja na mwanachama wa UDA au wakili wa Mahakama Kuu ya Kenya ili kuwawakilisha.

Uteuzi wa mchujo wa UDA ulianza Alhamisi, Aprili 14.

Katika machafuko ya Embu, lori lililokuwa likisafirisha nyenzo za uteuzi ziliibiwa Jumatano na masanduku ya kura na karatasi kuteketezwa.

Wawaniaji wa Embu awali walikuwa wamehutubia vyombo vya habari wakipuuzilia mbali madai kuhusu ripoti za mipango ya wizi.