Chama cha Wiper kinamtaka Kalonzo arudi Azimio

Muhtasari
  • Viongozi hao walimtaka Kalonzo kutumia mbinu zote za kutatua mizozo ndani ya chama cha Azimio la Umoja One Kenya
KINARA WA WIPER KALONZO MUSYOKA
Image: WILFRED NYANGARESI

Kiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka ameshawishiwa na maafisa wa chama kufikiria upya uamuzi wake wa kuwania urais.

Azimio hilo lilifikiwa wakati wa mkutano wa wajumbe huko Stoni Athi kaunti ya Machakos mnamo Jumatatu.

Viongozi hao walimtaka Kalonzo kutumia mbinu zote za kutatua mizozo ndani ya chama cha Azimio la Umoja One Kenya.

"Kuna utaratibu wa kusuluhisha mizozo chini ya muungano huo, kwa hivyo tunamwomba kiongozi wa chama chetu tufikirie uwezekano wa kuwa na majadiliano zaidi kuhusu mpango huu wa muungano," katibu mratibu Robert Mbui alisema.

Kalonzo anasemekana kuwa nje ya nchi kwa safari ya kibinafsi ya Uingereza.

Mbui alisema sababu iliyofanya chama cha Wiper kuamua kujiondoa Azimio na kutangaza kuwa Kalonzo atawania kiti cha urais ni kwa sababu hapo awali hakukuwa na nafasi ya majadiliano. chama hata kama Kalonzo Jumatatu aliwasilisha sahihi za wafuasi wanaounga mkono azma yake ya urais kwa IEBC.

"Kwa sababu tayari tulikuwa tumekubali kufanya kazi chini ya Azimio One Kenya Alliance, ni wakati muafaka kwamba tumalizie chaguzi zote ambazo zilikuwa zinapatikana," Mbui alisema.