Ngilu hatatetea kiti chake cha ugavana,Raila asema

Muhtasari
  • Raila aliwataka wakazi wa Kitui katika ziara ya kampeni kuchagua kati ya David Musila wa Jubilee na Julius Malombe wa Wiper
Gavana wa Kitui Charity Ngilu
Image: Musembi Nzengu

Gavana wa Kitui Charity Ngilu hatatetea kiti chake mnamo Agosti 9.

Kinara wa ODM Raila Odinga anasema Ngilu atapewa nafasi katika utawala wake.

Raila aliwataka wakazi wa Kitui katika ziara ya kampeni kuchagua kati ya David Musila wa Jubilee na Julius Malombe wa Wiper.

“Utakayemchagua awe Malombe au Musila, itakuwa wewe kuamua kwa sababu tunataka kupeleka Ngilu Nairobi,” Raila alisema.

Aliongeza kuwa utawala wake, iwapo atashinda kura ya Agosti, utahakikisha kaunti zimetengewa zaidi ya asilimia 35 ya sehemu ya mapato. Kuhusu chaguzi za chama, kiongozi huyo wa ODM alisema wakazi walikuwa huru kuchagua mgombeaji yeyote kutoka 26 wanaounda chama cha muungano cha Azimio la Umoja.

"Tuna Jubilee, ODM, Narc, Narc Kenya katika timu ya vyama 26... Ni nyinyi kuamua ni nani wa kumpigia kura miongoni mwa vyama kwani sote tuko Azimio," akasema.