Kigame ana digrii-Miguna atuma ujumbe huu kwa IEBC

Muhtasari
  • Reuben Kigame alipinga Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) kueleza ni kwa nini alizuiwa kushiriki katika Uchaguzi Mkuu ujao wa Agosti 9
Image: TWITTER// MIGUNA MIGUNA

Dkt. Miguna Miguna amedokeza kupitia ukurasa wake rasmi wa twitter akiitaka IEBC Kenya kumwidhinisha  Mgombea urais Mhe. Reuben Kigame kuwania uchaguzi mkuu wa Agosti 9.

Kulingana naye Reuben Kigame ana digrii mbili za kweli ambazo baadhi ya mgombeaji urais ambaye IEBC Kenya ilimwidhinisha hakuwa nazo.

"Kwa nini wanamzuia Reuben Kigame kuwa kwenye kinyang'anyiro cha urais? Reuben Kigame ana digrii 2 za kweli Na ana sahihi kutoka kaunti 28. IEBC Kenya lazima imwidhinishe Reuben Kigame" . Dkt. Miguna Miguna aliandika.

Wakenya wengi pia wanashangaa kwa nini Reuben Kigame hakuruhusiwa kuwania uchaguzi wa urais wa Agosti 9.

Reuben Kigame alipinga Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) kueleza ni kwa nini alizuiwa kushiriki katika Uchaguzi Mkuu ujao wa Agosti 9.

Akitumia ukurasa waketwitter mnamo Jumatatu, Juni 6, Kigame alieleza kwa kina matukio yaliyojiri kati ya Mei 16 alipotangazwa kwenye gazeti la serikali kama mgombea Urais hadi Mei 30 alipofungiwa nje ya kinyang'anyiro hicho.