Mungu halali ata Mkini Dhulumu Watu Wa Mathare Wameamua-Bahati amwambia Sifuna

Alidai kuwa umaarufu wake ulitishia wale wanaopinga ombi lake na kuwafanya kumkataa.

Muhtasari
  • Msanii huyo alikuwa amefika tu kwenye mkutano ulioandaliwa na viongozi wakuu wa muungano wa Azimio Nairobi alipofurushwa kwa nguvu
Kelvin Bahati Kioko anayelenga ubunge Mathare kupitia chama cha Jubilee
Msanii Bahati Kelvin Bahati Kioko anayelenga ubunge Mathare kupitia chama cha Jubilee
Image: Instagram screenshot

Mwimbaji Kelvin Bahati Kioko ametoa imani kwamba wapiga kura wa Mathare watamchagua kuwa mbunge katika uchaguzi wa Agosti 9.

Matamshi yake yanakuja baada ya kukasirishwa na kufukuzwa kutoka kwa maandamano ya Azimio katika eneo bunge la Mathare.

Msanii huyo alikuwa amefika tu kwenye mkutano ulioandaliwa na viongozi wakuu wa muungano wa Azimio Nairobi alipofurushwa kwa nguvu.

Akijibu kisa hicho, Bahati sasa anasema hataogopa kutendewa vibaya.

Alisema atasalia kwenye kura hadi mwisho kwani alishikilia kuwa anafurahia kuungwa mkono na wakaazi wa Mathare. Bahati alimkashifu SG Edwin Sifuna wa ODM kwa masaibu yaliyompata Jumatatu.

Alidai kuwa umaarufu wake ulitishia wale wanaopinga ombi lake na kuwafanya kumkataa.

"When Sifana and his Loosing Friend Saw THE INCOMING MATHARE MP - BAHATI KIOKO has arrived and the Crowd was Demanding to hear Me speak... They Decided to End the Meeting Pre- Maturely Against the Will of the People 🙂 Lakini MUNGU HALALI; ata Mkini Dhulumu Watu Wa Mathare Wameamua Kura Watapea Mtoto Wa Mathare 🙏 Lakini Mbona hawa Wazee Wote wanakasirishwa nahuyu Kijana Mdogo??? 🤣🤣🤣 #WhatGodHasBlessedNoMancanCurse,"Bahati alisema.