Naibu Rais William Ruto ashiriki mdahalo wa urais

Mgombea urais wa muungano wa Azimio Raila Odinga hajawasili

Muhtasari

•Mdahalo huo unapeperushwa moja kwa moja kwenye vituo vyote vya TV na redio.

• Ruto aliwasili akiandamana na mkewe na iwafuasi wake.

Mdahalo wa Urais ambao umekuwa ukisubiriwa kwa hamu na gamu hatimaye umengóa nanga.

Mdahalo huo unapeperushwa moja kwa moja kwenye vituo vyote vya televisheni na redio kote nchini.

Naibu rais William Ruto anaendelea kueleza wakenya mambo ambayo analenga kuwafanyia.

Mgombea urais wa muungano wa Azimio One Kenya Raila Odinga alitarajiwa kushiriki mdahalo na Ruto lakini bado hawajawasili.

Awali mgombea urais wa Chama cha Roots George Wajackoyah alitaja kutotendewa haki akisema wagombeaji wote wanne wangepaswa kuwekwa pamoja kushiriki katika mdahalo huo pamoja.

Baada ya wandalizi kudinda kutimiza matakwa yake, Wajakoya alijiondoa kutoka mdahalo huo na kumuacha mgombea urais wa chama cha Agano David Waihiga Mwaure kujadili maswala yake pekee yake.