Kakamega, Mombasa kufanya uchaguzi wa ugavana Agosti 23

Karatasi za kura za viti hivyo zilikuwa na picha na maelezo zisizo ya wagombeaji zisizo sawa.

Muhtasari

•Uchaguzi huo ulisitishwa pamoja na kura za wabunge huko Kacheliba na Pokot Kusini kutokana na mkanganyiko wa karatasi za kura.

•Kufikia mwisho wa upigaji kura saa kumi na moja jioni, Wanderi alisema Wakenya milioni 12,065,803 walinaswa kwenye KIEMS.

Mpiga kura akipiga kura katika kituo cha Shule ya Msingi ya Umoja. Upigaji kura ulianza vizuri katika sehemu nyingi za Nakuru
Mpiga kura akipiga kura katika kituo cha Shule ya Msingi ya Umoja. Upigaji kura ulianza vizuri katika sehemu nyingi za Nakuru
Image: NYAKERI KAIRIRE

Uchaguzi wa ugavana Kakamega na Mombasa utafanyika Agosti 23.

Uchaguzi huo ulisitishwa pamoja na kura za wabunge huko Kacheliba na Pokot Kusini kutokana na mkanganyiko wa karatasi za kura.

Mnamo Jumatatu mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati alisema karatasi za kura za viti hivyo zilikuwa na picha na maelezo zisizo ya wagombeaji zisizo sawa.

Jumanne jioni kamishna wa IEBC Francis Wanderi alisema kwamba uchaguzi huo pia utafanyika Kitui Rural na Rongai, kaunti ya Nakuru.

Hata hivyo, alisema wapiga kura katika eneo la Eldas wanapaswa kujiandaa kupiga kura Jumatano, Agosti 10 kuanzia saa kumi na mbili asubuhi.

Kufikia mwisho wa upigaji kura saa kumi na moja jioni, Wanderi alisema Wakenya milioni 12,065,803 walinaswa kwenye vifaa vya KIEMS kama walipiga kura.

Alisema idadi hiyo inawakilisha asilimia 56.17 ukiondoa wale waliotambuliwa kwa mikono.