(+PICHA) Matukio katika kituo cha kupiga kura cha Old Kibra Raila Akipiga Kura

Raila alifika kituoni hapo dakika za 10.30 asubuhi kwa mapokezi makubwa ya wafuasi wake.

Muhtasari

• Waziri Mkuu huyo wa zamani hakuzungumza na vyombo vya habari baada ya kupiga kura ilivyotarajiwa na wengi na badala yake aliamua kuondoka.

Kiongozi wa chama cha ODM Raila Odinga akipiga kura katika kituo cha shule ya msingi ya Old Kibera mnamo Agosti 9, 2022.
Kiongozi wa chama cha ODM Raila Odinga akipiga kura katika kituo cha shule ya msingi ya Old Kibera mnamo Agosti 9, 2022.
Image: ENOS TECHE

Raila aliwasili pamoja na mkewe Ida ambaye pia alipiga kura katika Kituo cha shule ya msingi ya Old Kibra na kupokelewa kwa shangwe na mbwembwe kutoka makumi ya wafuasi wake waliokuwa wamefurika katika kituo hicho.

Wana usalama walikuwa na wakati mgumu kudhibiti umati mkubwa uliojitokeza kumpokea.

Waziri Mkuu huyo wa zamani hakuzungumza na vyombo vya habari baada ya kupiga kura ilivyotarajiwa na wengi na badala yake aliamua kuondoka.

Hizi ni baadhi ya picha ambazo tulipata kukuandalia kutoka kwa tukio hilo la kihistoria waziri mkuu wa zamani akipiga kura yake, huku akiwa na imani kwamba alionesha kama mfano kwa wafuasi wake pia kumpigia kura kama mrithi wa rais Kenyatta.

Picha: ENOS TECHE
Picha: ENOS TECHE
Picha: ENOS TECHE
Picha: ENOS TECHE
Picha: ENOS TECHE
Picha: ENOS TECHE