Gladys Wanga ambwaga chini Kidero katika kinyang'anyiro cha ugavana Homa Bay

Wanga sasa atamrithi Cyprian Awiti.

Muhtasari

•Wanga alimshinda mpinzani wake Evans Kidero ambaye aliibuka wa pili kwa kura 154,182. Kidero alikuwa mgombea huru

Gavana wa Homa Bay aliyechaguliwa kwa tikiti ya ODM Gladys Wanga katika Shule ya Msingi ya Alara Korayo eneo bunge la Rangwe mnamo Agosti 9, 2022.
Gavana wa Homa Bay aliyechaguliwa kwa tikiti ya ODM Gladys Wanga katika Shule ya Msingi ya Alara Korayo eneo bunge la Rangwe mnamo Agosti 9, 2022.
Image: ROBERT OMOLLO

Mwakilishi wa Wanawake wa Homa Bay anayeondoka Gladys Wanga ameshinda kiti cha ugavana wa kaunti hiyo baada ya kupata kura 244,559. 

Mgombea huyo wa ODM alimshinda mpinzani wake Evans Kidero ambaye aliibuka wa pili kwa kura 154,182. Kidero alikuwa mgombea huru. 

Wanga sasa atamrithi Cyprian Awiti.

Siku ya Jumanne, viongozi hao wawili waliapa kukubali matokeo ya uchaguzi.

Wanga amehudumu katika kaunti hiyo kama Mbunge Mwanamke kwa muhula mmoja, baada ya kuchaguliwa mwaka wa 2017.