Ruto ashinda katika eneo bunge la Igembe kaunti ya Meru

Ruto alipata kura 45,497 dhidi ya mwenzake wa Azimio Raila Odinga aliyepata 13,343.

Muhtasari
  • Mgombea urais wa UDA William Ruto ameshinda eneo bunge la Igembe ya Kati, Kaunti ya Meru
Naibu rais William Ruto
Naibu rais William Ruto
Image: Facebook//WilliamSamoeiRuto

Mgombea urais wa UDA William Ruto ameshinda eneo bunge la Igembe ya Kati, Kaunti ya Meru.

Ruto alipata kura 45,497 dhidi ya mwenzake wa Azimio Raila Odinga aliyepata 13,343.

George Wajackoya wa chama cha Roots alipata kura 294 huku David Mwaure wa chama cha Agano akipata kura 165.

Idadi ya waliojiandikisha kupiga kura ilikuwa 93,471.

Kulikuwa na kura halali 59,299 katika Igembe ya Kati na kura 438 zilizokataliwa.

Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) lazima ithibitishe Fomu 34B kutoka maeneobunge 290 na matokeo ya diaspora kabla ya kutangaza mshindi.